July 2, 2021


 NYOTA wawili wa Simba kesho wanatarajia kuukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa. 


Kwa mujibu wa Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola amesema kuwa kiujumla maandalizi yapo tayari kwa ajili ya mchezo huo licha ya kuwakosa wachezaji hao wawili.

Matola amesema:-"Ni Jonas Mkude ambaye matatizo yake yanajulikana pamoja na Ibrahim Ajibu ambaye anasumbuliwa na Malaria.

"Mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti kwa kuwa kila kitu kipo sawa na wachezaji wanahitaji ushindi, maandalizi kiujumla yapo vizuri" amesema.

Simba ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikiwa na pointi 73 na Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 67.

Mkude alisimamishwa na Kamati ya nidhamu ya Simba kutokana na tatizo la kinidhamu ambapo anatakiwa kwenda kufanyiwa vipimo vya akili.

Kuhusu suala lake la kufanyiwa vipio Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema kuwa hilo suala linasimamiwa na kamati yenyewe.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic