July 2, 2021

 


RAZACK Siwa, Kocha wa Makipa amesema kuwa timu ya Yanga ni bora na inawachezaji wazuri watakaoipa matokeo chanya.

Kesho Julai 3, Yanga itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Simba  katika mchezo wa ligi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Siwa amesema kuwa wanaamini uimara walio nao hivyo watapambana kupata matokeo mbele ya Simba.

"Moja ya timu bora na Yanga pia ni mojawapo hivyo kuelekea katika mchezo wetu dhidi ya Simba hatuna mashaka.

"Imani yetu nikuona kwamba tunapata ushindi,  mashabiki wajitokeze kwa wingi ili kutupa sapoti," amesema.

Katika mchezo wa mzunguko wa awali, ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 1-1 Simba ambapo watupiaji walikuwa ni Michael Sarpong na Joash Onyango.

Na matokeo hayo yaliwafanya watani hao wa jadi wagawane pointi mojamoja.

Katika msimamo Yanga ipo nafasi ya  pili na ina pointi 67 huku Simba ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 73.

Yanga inapambana kurejesha nguvu ya kutwaa ubingwa pamoja na kuwania nafasi ya pili huku Simba ikihitaji pointi tatu kutangazwa kuwa mabingwa mara ya nne mfululizo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic