July 5, 2021


 UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa watani wao wa jadi Simba, washukuru wamepona kipigo kizito kwa kuwa ilibidi wachapwe zaidi ya bao moja walipokutana kwenye mchezo wao Julai 3.

Ni Zawad Mauya ambaye alipachika bao la ushindi kwa Yanga dk 12 lililompoteza mwelekeo kipa namba moja Aishi Manula kwa sababu liligongana na kifua cha beki Shomari Kapombe aliyekuwa kwenye harakati za kuokoa.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonion Nugaz amesema kuwa walistahili ushindi kwenye mchezo huo na ilibaki kidogo washinda mabao matatu kwa bila mbele ya Simba.

"Watani wetu washukuru tu kwamba walifungwa bao moja lakini ilibidi wafungwe zaidi ya mabao matatu kwa kuwa tulikuwa imara na bora kwenye mchezo wetu.

"Yanga tuna wachezaji wa kazikazi, wakiambiwa sasa tunakwenda kufanya kazi inakuwa mwanzo mwisho kukomaa kutafuta matokeo hivyo hakuna namna nyingine ambayo wangeepuka kufungwa mbele yetu," amesema.

Kwenye msimamo wa ligi, Yanga ipo nafasi ya pili ina pointi 70 baada ya kucheza mechi 32 imebakiwa na mechi mbili mkononi.

Mtani wake wa jadi, Simba yupo nafasi ya kwanza na pointi zake ni 73 baada ya kucheza jumla ya mechi 30.

6 COMMENTS:

  1. Yanga hata aibu wanakosa, simba kanyimwa penati mbili dhahiri, ingekuwa wao ndio imetokea hivyo wangekuwa wameenda hadi fifa kulalamika. Mpira acheze mchawi mpili furaha apate yanga, ajabu na kweli.

    ReplyDelete
  2. Wazee wa wakazi gani? Akina Dalali wako wapi Simba inanyanyaswa kichawi.

    ReplyDelete
  3. wawa kashika kwenye boksi kimya, boko alistahili kadi nyekundu kimya, halafu jitu la ute linakurupuka tu huko eti penati mbili, hapo tulizuia paka tu asiingizwe uwanjan mnyama chali

    ReplyDelete
  4. Mlitaka nini mabao matatu nini kilichokuzuwieni kuyapaaataa???

    ReplyDelete
  5. Nikicheki comenti za washabiki wa thimba nacheka sana yaani dunia inakwenda kasi.mnadai penati sio 7 bila?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic