July 5, 2021


 ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Ihefu FC ya Mbeya ana fupa gumu la kupasua ili kupata pointi sita muhimu zitakazompa nafasi ya kuamua hatma ya timu hiyo kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2021/22.

Imecheza mechi 32 ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 35 kibindoni, katika nafasi ambayo ipo ni nyekundu kwake kwani ikipoteza mechi zake zilizobaki inaweza kushuka mazima mpaka Ligi Daraja la Kwanza.

Mchezo wake ujao wa ligi ni dhidi ya Yanga itakuwa Julai 14, Uwanja wa Mkapa ambapo kwenye mchezo wa awali walipokutana Uwanja wa Sokoine ubao ulisoma Ihefu 0-3 Yanga na KMC, Julai 18 Uwanja wa Uhuru.

Mchezo wa kwanza walipokutana na KMC, Ihefu ilishinda bao 1-0 ilikuwa ni Desemba 19 hivyo haitakuwa kazi nyepesi kwao kupata ushindi kwa kuwa KMC inahitaji kumaliza ndani ya nne bora.

Katwila aliiambia Spoti Xtra kuwa wanatambua ushindani ni mkubwa ila aliwaambia wachezaji kuwa lazima wajitume na kucheza bila kukata tamaa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic