July 5, 2021


UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba kuelekea kwenye mchezo wao ujao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba watawafunga bila kuwaogopa na kutwaa taji la pili miguuni mwao.

Julai 3 kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi, ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 0-1 Yanga. Ilikuwa ni zawadi ya mashabiki wa Yanga kutoka mguu wa Zawadi Mauya aliyefunga bao la mapema dk 12.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela ameweka wazi kwamba hawana mashaka na watani zao wa jadi wakikutana tena wanawafunga.
 
"Hatuna mashaka nao tukikutana nao Julai 25, tunawafunga tena, uzuri ni kwamba tuna timu imara na kila mmoja analitambua hilo.

"Mbinu za mwalimu wetu zinaonekana na kila mtu anakubali hivyo wakati ujao imani yangu ni kuona kwamba tunaongeza kasi zaidi na kuendelea kujiamini, mashabiki waendelee kutupa sapoti" amesema.


Mchezo huo ni wa fainali ya Kombe la Shirikisho unatarajiwa kuchezwa Julai 25, Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Tayari Yanga ilitwaa taji moja mguuni mwa Simba lilikuwa ni lile la Mapinduzi ambalo lilifanyika huko Zanzibar.

7 COMMENTS:

  1. Chonde chonde viongozi hivi sasa tuna firaha sana. Lakini jana kuna mtu wangu kaniambia kuwa mchezo wote wa juzi ilikuwa refa ndio ngao yetu. Sasa mimi naogopa ikija tunawakilisha taifa tutapata tabu sana. Tutatolewa mapema. Kwa hicyo usajili. Mishahara ya wachezaji na mishahara ya makocha. Wala sisi madhabiki hatutaki kuona timu yetu inabebwa. Tucheze mpira tutambe Afrika kama wao Simba ila sisi safari hii tuchukuwe kombe la CAF

    ReplyDelete
  2. Hakuna cha mbinu za mwalimu wala nini ni mbinu za mzee mpili na refa wenu. Mpira wa yanga uko chini mno ulilinganisha na simba, janja janja tuu nje ya uwanja

    ReplyDelete
  3. Semeni tu kwamba mlidhibitiwa janja ya kutumia madawa na figisu ya kupiuliza vyumbani, mastaa wenu wakawa nyambenyambe daadeki nyie

    ReplyDelete
  4. Wewe utakuwa una shida, hoyo ishu ya kupuluza dawa miaka sasa mnasema mmeshindwa vipi kuwakata ili kuwe na ushahidi? Unaimba tuu kama zezeta vile

    ReplyDelete
  5. Kila siku siyo jumapili, tukutane faini tuwagonge Simba hatuna msalia mtume

    Mjinga atabisha hpo

    ReplyDelete
  6. Nina imani kuwa mwandembwa atachezesha tena Julai 25 ili mpate ushindi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic