July 6, 2021


 HASSAN Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa ni suala la muda tu kwa timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara huku wakitaja siku ya kuchukua ubingwa.

Yanga ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi zake 70 baada ya kucheza mechi 32 huku Simba ambao ni mabingwa watetezi wakiwa nafasi ya kwanza na wana pointi 73.

Bumbuli amesema kuwa kwa namna yoyote ile wao ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara kwa msimu huu na hilo litakuwa wazi baada ya wao kumaliza mechi zao mbili ambazo zimebaki.

Bumbuli amesema :-"Wakibahatisha safari hii wakibahatisha kushinda, wakachukua hapa itakuwa ni bahati yao. Kwanza huu msimu sisi mabingwa niulize kuanzia tarehe 13 mwezi huu wa 7. Mpaka tarehe 23 mwezi wa saba tutakuwa mabingwa.

"Tuna mechi mbili zimebaki ambazo ni dhidi ya Ihefu na Dodoma Jiji, baada ya kumaliza mechi hizo hapo mtajua kwamba nani anakuwa bingwa, sisi hatuna wasiwasi na ubingwa maana hawana namna ya kuweza kuchukua ubingwa," amesema Bumbuli.

 Chanzo:Azam TV

11 COMMENTS:

  1. Haeleweki, labda kama anaamini uchawi waliofanya utawasaidia simba kupoteza mechi zote zilizobaki. Ikitokea hivyo nitaamini mchawi waliyempata anawalipa, na watakuwa mabingwa wa kichawi sio mpira. Vinginevyo yanga kuwa bingwa ngumu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mikia bhana mbona kutwa kila siku kulalamika tu..... Mapaka yenu siku hizi hamyatumii aiseeeee???? Na nyie mna mapaka Kama vipi fanyeni mnayoyajua......

      Delete
  2. We unaye jiita Unknown unadhani mpira Una uchawi c Ungeona Timu za Africa zinge chukua ubingwa acha hizo imani zako potofu mpira kujiandaa na kuya sikiliza maelekezo ya kocha bhas kama game plan ime feli bhas Mikia mna matatizo sana sana

    ReplyDelete
  3. Chizi c lazima aokoke makopo! Ni chizi peke yake ndo anaamini Utopolo watabeba ubingwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Uelewa mdogo, hapo kuna issue ndani ya issue, mikia jisahaulisheni tu

      Delete
  4. Bumbui,unafikiria ya 2010 wakati Moro United iliyokuwa ikiongozwa na Mosha!?umekosea,hii ni Simba.Unategemea pointi zitatoka Fifa?

    ReplyDelete
  5. Mikia fc Hata game ya Yanga mlisema mtashinda lkn mmeangukia pua, na bado mtaumia mpaka mjifunze kuheshimu team pinzani

    ReplyDelete
  6. Umemzidi mwenzio michezo miwili,kakuzidi mpaka magoli,halafu kakuzidi point kisha unasema wewe utakuwa bingwa?hebu pale kaunda badala ya kufuga mamba na vyura hebu fugeni japo kambare wanaweza kuwapa akili kidogo

    ReplyDelete
  7. Jamani simba hawaamin hadi sas

    ReplyDelete
  8. Simba nitimu kubwa saw hatukatai lakini nitimu kubwa kwa timu ndogo ..sio kama yanga ,,,yanga timu kubwa sana

    ReplyDelete
  9. Mwamsheni Bumbuli anaota ndoto mbaya. Ubingwa n wetu mara 10 mfululizo, tageti hyo na ndo kwaaanza!! wa 4.Aahahahaha! Watoto wa MSIMBAZ!!!!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic