UONGOZI wa Klabu
ya Yanga, umempeleka Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara kwenye Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi kutokana na kauli yake ya kuwaita wachezaji
wao wakuokotwa.
Manara
aliyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Juni 30, mwaka
huu, kwenye Ukumbi wa Serena Hotel, Dar wakati Simba ikijiandaa na mchezo wa
ligi dhidi ya Yanga.
Manara
kwenye mkutano huo alisema: “Yaani Simba ina Chama, Bwalya, Bocco ukachukue
watu wameokotwaokotwa halafu useme wanaweza kutufunga, hiyo haiwezekani.”
Chanzo
kutoka Yanga, kimeliambia Championi Jumamosi, kuwa: “Baada ya Ofisa Habari wa Simba,
Haji Manara kuongea vibaya kwenye mkutano na waandishi wa habari, na kuwakandia
wachezaji wa Yanga kuwa ni wa kuokotwa, viongozi wamechukia na kuipeleke kesi
hiyo TFF na Bodi ya Ligi kwa ajili ya kuitolea hukumu.
“Mwanzo
walitaka kuipeleka mahakamani kabisa wakaona waanzie huku ila na TFF wenyewe
wanataka wampige faini kimya kimya,” alisema mtoa taarifa huyo.
Kwa upande
wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo,
alipotafutwa alisema kuwa: “Sipo ofisini kwa sasa, hivyo sifahamu juu ya
malalamiko hayo ila nitakapoenda ndio nitajua.”
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa alisema: "Ni kweli
tumepeleka malalamiko yetu TFF juu ya kauli ya Manara.”
Chanzo:Championi
Mmmmhhh!! Huo utani wa jadi ndo ushakufa au wivu tu kuona timu flani inafanikiwa zaidi... Inaonesha hata ile mechi Kama Utopolo ndo wangenyimwa zile penati sa hz wangekuwa CAS au FIFA kabisa
ReplyDeleteMavi ya mwamedi....umefanikiwa nini...kuingia na mapaka uwanjani au....yaani mimba tumewapa ila bado mnaongeaongea.....au ndo dalili za mimba hizo
DeleteNina wasiwasi na akili za watu wa yanga. Nina hakika ni makanjanja kama alivyotuhakikishia kocha wao alipoongea akiwa iringa
DeleteWakuokotwa kweli hata marefarii wetu ni wakuokotwa pia sijui kwanini MANARA alishindwa kuongozea na hilo la marefa.Na kwa marefa Hawa watanzania Simba ataendelea kungara tu kimataifa na kuteseka kwenye ligi yetu.Yule Mwandembwa wakuchezesha mchangani sio proffesional football kwenye TV.CAF NA FIFA Wakiangalia ujinga wanaofanya marefa wetu hawaamini jinsi sisi watanzania tumekosa umakini kwenye vitu vya msingi.
DeleteUbingwa Mara nne mfululizo, kimataifa robo fainali mara mbili ndani ya miaka 3. Bado unasema hawajafanikiwa..... kweli nyie ni Utopolo na mkibaki na akili zenu hzo za kizamani mtaishia hvyo hvyo kila mwaka
DeleteDuuh!! Uongozi wa hiyo timu unatia shaka
ReplyDeleteSimba kuweni makini hayo mambo yasiwatoe kwenye reli, yatatueni kadiri inavyostahili ili mtimize malengo yenu ya msimu huu
ReplyDeleteWameonja ushindi sasa wataanza vituko vingi sana
ReplyDeleteToka last year mpaka now MIKIA WAMEFUNGWA MARA 3 AFU WENYEWE WETUFUNGA MARA MOJA...Tumia akili unapocomment kijana
DeleteYanga insignia simba kichawi lakini simba inakuwa katika 10 bora Africa nzima kisayansi na ndio inaheshimika zaidi Afrika. Na wapenzi wake sio mambumhu kama wale walioitwa mambumbu na kocha wao
DeleteFilosofia yao ni kujaribu eti kuwapa wasiwasi Simba ili wapare ushindi mwengine
ReplyDeleteHivi tunaekekea wapi? Yanga maana huo ndio utani wa kumbukeni kipindi Cha Jeri muro tulivyokuwa tunawatania.
ReplyDeleteHapana huo sio utani Bali unatengeneza chuki baina ya hiz team mbili
ReplyDelete