July 5, 2021


 IKIWA ni mara ya kwanza kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu kuibuka Uwanja wa Mkapa, alishuhudia Yanga wakisepa na ushindi mbele ya watani wao wa jadi.

Zawad Mauya ingizo jipya ndani ya Yanga, ndiye aliyeibuka shujaa kwa kumtungua kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula, Julai 3 Uwanja wa Mkapa aliibuka shujaa kwa kuzima ndoto za mabingwa watetezi Simba kutangazwa kuwa mabingwa mara ya nne kwenye Ligi Kuu Bara.

Ingizo hilo jipya kutoka kikosi cha Kagera Sugar kiliibuka hapo kimyakimya baada ya mabosi wa Yanga kukosa huduma ya Awesu Awesu ambaye yupo zake ndani ya kikosi cha Azam FC.


Ni bao lake la kwanza kufunga ndani ya ligi akiwa na Yanga na amefunga mbele ya timu kubwa ambayo ni Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes na ilikuwa ni dk ya 11.


Ushindi huo unaifanya Yanga kutibua rekodi ya Gomes ambaye alikuwa amekiongoza kikosi hicho kwenye jumla ya mechi 14 bila kufungwa ila juzi mechi ya 15 aliyeyusha mazima pointi tatu.


Mechi zake


Mechi 17 ambazo amecheza ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.


Jumla ametumia dk 874

Katika mechi zake zote ndani ya Yanga msimu wa 2020/21 ameyeyusha jumla dk 874.

Dabi ya kwanza

Dabi ya kwanza hakuyeyusha dk 45 ila alianzia benchi na alipewa jumla ya dk 8 ilikuwa zama za Cedric Kaze na ubao ulikamilika kwa kusoma Yanga 1-1 Simba, Uwanja wa Mkapa,Novemba 7.

Mabao mawili yalifungwa na wageni ambapo kwa Yanga alikuwa ni Michael Sarpong raia wa Ghana alipachika bao kwa mkwaju wa penalti na lile la Simba lilifungwa na Joash Onyango raia wa Kenya ambaye alisababisha pia penalti kwa kumchezea faulo Tuisila Kisinda raia wa Congo.


Dk 90 mechi kiduchu

Yeye sio chaguo la kwanza ndani ya Yanga tangu enzi za Kaze na mpaka sasa zama za Nabi ambapo jumla ni mechi  sita aliyeyusha dk zote 90.


Hizi hapa Mauya aliyeyusha jumla ya dk 90:-Mtibwa Sugar 0-1 Yanga, Uwanja wa Jamhuri,dk 90, Morogoro. Gwambina 0-0 Yanga, Novemba 3, Uwanja wa Gwambina Complex, dk 90. Namungo 0-0 Yanga, Uwanja wa Majaliwa, dk 90, Mei 15.Ruvu Shooting 2-3 Yanga, Uwanja wa Mkapa, dk 90. Yanga 3-2 Mwadui FC, Uwanja wa Mkapa, Juni 20 dk 90. Simba 0-1 Yanga, Julai 3, Uwanja wa Mkapa.

Mechi zake ambazo hakuyeyusha dk 90

Yanga 1-1 Tanzania Prisons dk 75 ilikuwa Septemba 6, Uwanja wa Mkapa. Kagera Sugar 0-1 Yanga, dk 83, Uwanja wa Kaitaba, Septemba 16. Yanga 3-0 Coastal Union, Oktoba 3, dk 45 Uwanja wa Mkapa. Yanga 1-0 Polisi Tanzania, Uwanja wa Uhuru, dk 13.


Biashara United 0-1 Yanga, Uwanja wa Karume, dk 1. Yanga 1-0 JKT Tanzania, Uwanja wa Mkapa dk 36, Novemba 28. Yanga 3-3 Kagera Sugar, Uwanja wa Mkapa dk 45. Polisi Tanzania 1-1 Yanga, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, dk 17.


KMC 1-2 Yanga, Uwanja wa CCM Kirumba, dk 3. JKT Tanzania 0-2 Yanga, Uwanja wa Jamhuri Dodoma, dk 8.


 


 


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic