WAKATI timu mbalimbali zikiendelea na usajili wa kuimarisha vilabu vyao Uongozi wa timu ya Biashara United ya mkoani Mara kupitia kwa kocha wake Mkuu Patrick Odhiambo amesema malengo yake ni kusajili wachezaji 9.
Kocha huyo ameongeza kuwa wachezaji hao anaamini kwamba wataongeza nguvu katika kikosi chake kuelekea msimu ujao wa ligi unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Kocha Odhiambo amesema kuwa:”Ni kweli baada ya kuachana na wachezaji 14 kwa sasa najipanga kusajili jumla ya wachezaji 9 tu ambao watakuja kuongeza nguvu kwa hawa waliopo ili kwa msimu ujao tuwe na timu bora ambayo itaweza kupambana katika uwanja wowote na tukapata matokeo.
Hivi
karibuni Biashara iliachana na nyota wake wapatao 17 ambao hawakufanya vyema
katika kikosi hicho licha ya kumaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa
ligi hivyo kocha Odhiambo ambaye kwa sasa anasomea leseni A ya CAF amepanga
kusajili wachezaji 9 ambao watakuja kuziba pengo lililoachwa na wachezaji hao.








0 COMMENTS:
Post a Comment