KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Simba, Rally Bwalya amefunguka kuwa bado hajapewa taarifa yoyote ya kuhitajika na Wababe wa soka la Morocco, Moulodia Oujda na anasubiri Uongozi wa Simba juu ya dili hilo.
Vyanzo vya habari kutokea nchini Morocco vimeeleza kuwa klabu ya Moulidia imetuma ofa kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Simba, kwa ajili ya kuhitaji huduma ya kiungo huyo raia wa Zambia.
Bwalya aliyejiunga na Simba mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea, Power Dynamos ya Zambia amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja pekee ndani ya Simba katika mkataba wa miaka miwili aliosaini Simba.
Akizungumzia uwepo wa ofa hiyo, Bwalya amesema: “Mpaka sasa binafsi sijawasiliana na klabu yoyote kuhusiana na ishu ya kuondoka Simba, lakini pia viongozi wangu wa Simba hawajanipa taarifa ikiwa kuna ofa yoyote kwa ajili yangu.
“Lakini masuala ya usajili ni maamuzi ya Uongozi na kama
kutakuwa na chochote kutoka huko Morocco, au klabu nyingine basi wao wataweka
wazi kila kitu.”
Jamani tuachieni bwalya musiwamalize kabisa kabla pengo la kipenzi chetu konde boy halijapatikana mbadala kwel
ReplyDeleteTaarifa za wakuda hizi hazina ukweli wowote. Bwalyaa na Triple C bado wapo sana.
ReplyDeleteendelea kujidanganya mo anataka pesa kwan we hujuw mpira sasa ni biashara endapo wakifikia makubaliano atauzwa tu
ReplyDeleteUtauxwa wewe. ni kweli mpira ni pesa 2.b za morison zinawasajili wote wapya yanga nani akataeee
DeleteNi kweli atauzwa kikubwa watulee jembe lingine kama bwalya
ReplyDeletechama tayar berkane
ReplyDeleteHuo wote ni uzushi
ReplyDelete