August 22, 2021


 DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa anawaamini wachezaji wake na anajua kwamba watakuwa tofauti  kwa msimu ujao kutokana na maandalizi ambayo wanayafanya.



Wakiwa nchini Morocco,  jana Agosti 21 walicheza mchezo wa kirafiki na FAR Rabat na ngoma kukamilika 2-2 jambo ambalo limemfurahisha kocha huyo.


Unakuwa ni mchezo wa kwanza kwa Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara kucheza tangu walipoweka kambi nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2021/22.


Gomes amesema:"Nafurahishwa na namna ambavyo wachezaji wangu wamafanya ni furaha kwangu na kwao pia. Kwa hali ilivyo nadhani tutazidi kuwa bora zaidi.


"Bado tuna mwezi mmoja wa kufanya kazi na maandalizi zaidi hivyo bado tuna muda wa kujiaandaa kwa ajili ya msimu ujao na ninafurahishwa na kile ambacho wachezaji wanakifanya,".

8 COMMENTS:

  1. Chini ya kiwango Cha akili kufikiri kuwa timu lazima ishinde mechi zake zote hata zile za Bonaza. Kama hii ingekuwa mechi ya mashindano basi simba anafaida ya magoli ya ugenini na point mkononi.
    Utopolo hata kupata mechi ya kujipima nguvu wanashindwa.wamebaki kuisemea simba.

    ReplyDelete
  2. Pamoja na kuanza mazoezi mapema mlizidiwa katika mechi, mushukuru hiyo draw mliopata kwa goli la kuotea

    ReplyDelete
  3. Hiyo ni mechi ya kwanza ya majaribio tu ambapo kusudi ni kupima uwezo wa kila mchezaji na kutafuta forrmation sahihi wala sio wa kushinda kombe. Ikiwa hiyo ndio target ya Simba, target ta Far Rabat katika nechi hiyo ni kujitayarisha kwa kikosi chao kamili tena nyumbani. Usitaraji kuiona Simba katika majaribio ya kwanza kwa wingi wa wachezaji wapya kuonesha kiwango kile mlicho lala kwa goli moja na kulikosa kombe la Azam. Safari ndefu huanzia hatuwa moja

    ReplyDelete
  4. Utopolo mmepigwa goli 14 kwa 2. Hiyo haitatangazwa popote maana ni aibu

    ReplyDelete
  5. Huyo Utopolo anayesema timu imecheza chini ys kiwango timu yao imecheza na nani?Au anazungumzia goli 14 kwani ni kweli timu yao ilicheza chini ta kiwango. Toka waburuzwe kule Kigoma na kulazimishwa kushiriki kwa kubebwa (viti maalum).Mabingwa wanangojea raundi ya pili.Raundi ya kwanza mnaanza nyie na wachovu wenzenu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic