August 30, 2021




BAADA ya jana, Yanga kukamilisha kilele cha Wiki ya Mwananchi, Ofisa Habari wao Haji Manara muda wa kurejea nyumbani anasema kuwa alipata ajali mbaya ya gari.

Manara ambaye aliibuka Yanga akitokea Simba leo alikuwa na mahojiano na kituo cha E FM jambo ambalo limemfanya akwame kufika katika kituo hicho kwa ajili ya mahojiano.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram, Haji Manara aliweza kuwajibu E FM baada ya kuandika taarifa yenye kichwa cha habari, "Haji Haji'. 

Kupitia Ukurasa wake Rasmi wa Istagram, Manara ameandika:" Ndugu zangu EFM nawaomba radhi sana kwa kutofika kwenye kipindi asubuhi ya leo kama nilivyoahidi kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu.

"Usiku wa jana nilinusirika na ajali mbaya ya gari baada ya gari yangu kugongwa vibaya na kusababisha kuharibika vibaya gari yangu.

"Hadi kuja kulala ilikuwa ni mida mibaya ya usiku mkubwa na sikuweza kuamka mapema ili niwahi kipindi chenu alfajiri ya leo saa kumi na Mbili.

"Nawaomba tena radhi nyie na wasikilizaji na watazamaji wote. Mnisamehe sana na nimejisikia vibaya sana," .

11 COMMENTS:

  1. Muzee ya matukio na kiki, hachelewi kusema kakongwa na wabaya wake kumbe yeye ndio ana makosa

    ReplyDelete
  2. Pole sana Mungu akuvuwe kwa kila ovu

    ReplyDelete
  3. Achakulopoka wewe angegongwa ungefaidika na mini makokolo fc wananyege Sana mwakahuu mtakoma

    ReplyDelete
  4. Ni heri binaadamu kuishi kwa mapenzi na mafahamiano na kujiepusha na hasama kwa kila mtu kwasababu mahaba yanajenga na kuleta baraka na hasama inabomowa na kuleta mikosi

    ReplyDelete
  5. Kabisa Manara anayatengenezea maisha tension zisizo na ulazima. Inaweza kuwa ajali ya kweli watu wakadhani ni kiki tu. Unapo tamka hadharani fulani ni m'baya wangu.Na nanihii nae ni m'baya wangu. Watu fulani nawachukia, hii sio njia sahihi ya kujitafua umaarufu.Mbaya zaidi sio Siri anakwenda kupick mtu Kama Mao kuwa ni m'baya wake na anataka kumuonesha kuwa yeye ni nani? Ijulikane tu ukiamua kuanzisha vita Mo umeamua kuanzisha vita na Simba sports club yaani vita na watanzania kama millions 30 na zaidi ni serikali hiyo tayari. Unajua mtu hawezi akajitia kibri kwa kujificha kwenye mgongo wa Mungu kuwa yeye hamuogopi mtu isipokuwa Mungu.Huwezi jirusha kwenye Bwawa la Mamba bila ya dharura yeyote kwakuwa wewe huogopi kitu isipokuwa Mungu. Huko itakuwa ni kumjaribu Mungu na Mungu atakupa majaribio ya kweli kweli usije ukasema watu wanakuchukia.

    ReplyDelete
  6. Ajali feki ili kupata kiki.Huyu amekuwa kama Amber Rutty kutafuta kiki.Jana wapenzi wa Yanga walimzomea kumuonyesha kwamba wao sio wajinga.GSM ndio wamemleta Haji na sio viongozi wa Yanga.Ingekuwa Yanga wanajitegemea Haji asingekuwepo Yanga.

    ReplyDelete
  7. Hao nimikia fc washabiki wa yanga hawawezi kumzomea manara uongo

    ReplyDelete
  8. Mpira unajenga urafiki, kujuwana kwa jamii duniani kote wala haujengi chuki na uadui

    ReplyDelete
  9. M͟a͟k͟o͟k͟o͟l͟o͟ f͟c͟ m͟w͟a͟k͟a͟ h͟u͟u͟ m͟t͟a͟s͟e͟m͟a͟ t͟u͟

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic