August 5, 2021

 


MANCHESTER City leo Alhamisi wanapewa nafasi ya kumfanyia vipimo nyota wa timu ya Aston Villa Jack Grealish kwa ajili ya kuweza kukamilisha mchongo wa nahodha huyo kujiunga na timu hiyo ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu England.

Ikiwa dili lake la pauni milioni 100 litajibu basi litavunja rekodi ya uhamisho wa nyota Paul Pogba alipoibukia Manchester United msimu wa 2016 katika historia ya Uingereza kwenye masuala ya mpira hivi karibuni.

Manchester City walipeleka ofa yao Aston Villa Ijumaa na wameonesha nia ya kumpata nahodha huyo ambaye aliwahi kucheza na Mtanzania Mbwana Samatta kwenye timu hiyo ya Aston Villa.

Ni kwamba Paul Pogba usajili wake uligharimu pauni milioni 93.5 wakati akitoka Juventus na kujiunga na Manchester United mwaka 2016 hivyo City wanataka kuvunja rekodi.

Kiungo huyo pia awali alikuwa anahitajika na Manchester United ambapo kwa namna dili linavyokwenda huenda ataibuka City msimu ujao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic