August 4, 2021

OFISA Habari wa Simba Haji Manara amesema kuwa anawashukuru mashabiki, wachezaji, viongozi pamoja na wadau ambao walikuwa wakifanya naye kazi wakati alipokuwa Ofisa Habari wa Simba kabla ya kubwanga manyanga na kuwabwaga mashabiki kupitia Kundi la Simba HQ.

 Manara amesema kuwa sababu kubwa ya yeye kuondoka Simba ni mbili ambapo ya kwanza ni suala la biashara na ile ya pili ni suala la umaarufu.
 

 

6 COMMENTS:

  1. Simba walikuwa wapo right kumtumuwa Manara ndani ya Simba tena wamechelewa. Miongoni mwa watu wa hovyo kuwahi kuwahi kuwasikiliza nikiwa nikidhani ni watu makini. Hivyo kama KHAJI MANARA angekuwa Mwinyi Zahera jinsi alivyojitoa kuisaidia Yanga katika kipindi kigumu kwa hali na mali na kuja kutimuliwa Yanga Kama ingekuwa Manara ingekuwaje? Zahera Mkongomani huyu ila uzalendo wake kwa Yanga haukuwa na kipimo na baada ya kutokea yaliyotokea hatukumuona Zahera akiitisha preconference kuizodoa Yanga au uongozi wa Yanga.
    Dhahiri shahiri MANARA alikuwa anaihujumu simba kwenye mechi za Yanga,huyu hakuwahi kuwa na Mapenzi na simba ni Mnafiki. Mwenye mapenzi na Simba hawezi kuwa mtu mwenye tabia za Khaji Manara zidi Simba. Hao akina Ismail Aden Rage wamechezea simba amekulia Simba anazeekea Simba na kuna wakati alipata misukosuko mikubwa tu kutoka kwa wanachama wa simba lakini wakaishia kimya. Hao ndio wenye mapenzi na timu yao. Manara anapambana kuibomoa image ya Simba yupo very selfish Ila hatafanikiwa zaidi ya kujimaliza yeye mwenyewe. Huyu Mtu wanasimba wenye mapenzi ya kweli juu ya Simba wajue sie mwenzao na Yale yote aliokuwa akiyafanya ndani ya Simba kumbe haikuwa kwa ajili ya Simba Bali ilikuwa ni kwa ajili ya Manara.Aliwadanganya wanasimba vyakutosha kuwa anaipenda simba ni unafiki utupu,alikuwa akitumia simba kujipatia umaarufu baada ya kuupata umaarufu anakwenda kuiumbua Simba. Kama si Simba nani angemjua Khaji Manara? Mshenzi mkubwa huyu mkosefu wa fadhila. Hovyo kabisa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. UMETUMA. TUNAJUA JAMAA KUWEKA WATU SPECIAL KU COUNTER HOJA ZA MANARA. NAWAAMBIENI WANA SIMBA WENZANGU SOON TUTAMKUMBUKA MANARA

      Delete
    2. Kwa ujinga huu anaokuja nao hakuna atakae mkumbuka kamwe labda kwa mtu kama wewe usie na msimamo

      Delete
    3. Mpumbavu,
      Simba hawana haja ya kujibizana na Mpumbavu.Bila ya simba Nani angemjua Khaji Manara? Eti halafu mkuleo kawa mkubwa kuliko Simba? Anatukana mpaka muezeshaji wa klabu. Ogopa Sana na kamwe usimuamini mtu mwenye maneno mengi.

      Delete
  2. Manara alikuwa mamluki ndani ya Simba. Siku zote Mungu hamfichi Mnafiki ndani ya watu waliomuamini atajifichua yeye mwenyewe ndicho kilichokea kwa Manara. Alikuwa Msaliti Mamluki ndani ya Simba na Manara muda si mrefu atajutia anachoendelea kulifanyia bila ya kuguswa na Mtu.

    ReplyDelete
  3. Manala simba ilikupenda ila wewe hukuipenda kwa hiyo nenda ukafundishe madrasa kazi ya utangazaji imekushinda

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic