August 31, 2021


RASMI sasa Yusuph Mhilu ni mali ya Simba baada ya uhamisho wake kukamilika na mabosi wa Simba kuweka mkwanja mezani kwa ajili ya kuvunja mkataba wake.

Taarifa rasmi kutoka Kagera Sugar imeeleza namna hii:"Tumefikia makubaliano ya pande zote mbili (Kagera Sugar FC na Simba SC) juu ya uhamisho wa aliyekuwa mchezaji wetu Nyota Yusuph Valentine Mhilu kwa Dau la Tsh.40M.


"Yusuph Mhilu alisaini kandarasi ya miaka miwili kuitumikia Kagera Sugar Football Club mwaka jana 2020. Hivyo uhamisho huu wa Yusuph Mhilu kwenda Simba ni Uhamisho ambao umehusisha kuvunja mkataba wake wa mwaka mmoja uliosalia ndani ya Klabu ya Kagera Sugar.

"Tunamtakia kila la kheri huko aendako na Mungu amsimamie katika kukiendeleza kipaji chake,".

Usajili wa Mhilu kuibukia Simba ulikuwa ni wa ghafla baada ya viongozi wa Simba kumdaka mazimamazima Dar alipotoka na timu ya taifa ya Tanzania kwa vijana chini ya umri wa miaka 23 kushiriki Cecafa.

Alisaini dili la miaka mitatu jambo ambalo liliwafanya mabosi wa Kagera Sugar kushangazwa na suala hilo la utambulisho kwa kuwa hakukuwa na taarifa kwao.

Kwa taarifa hiyo ni wazi kwamba Mhilu msimu ujao atakuwa ndani ya Simba kuendelea kupambania namba.

5 COMMENTS:

  1. Mbona mnawadharau wachezaji wetu wazawa? Million 40 kwa Muhilu simba kakamuliwa vipi? Yaani Muhilu hana thamani ya million 40? Acheni utakataka wa uandishi.

    ReplyDelete
  2. Kuna watu wameumbuka hapa kwenye usajili wa Muhilu baada ya maneno meeeengi ya kuidhalilisha Simba kuwa haifuati taratibu inatumia ubabe blah blah blah walitamani hili suala la Muhilu liishie kwa kuingiza simba kwenye matatizo lakini Mungu siku zote hasimami upande wa wenye roho chafu za kubomoa. Sasa baada ya suala la Muhilu kwisha Salama wabaya wanashindwa kuandika positive juu ya suala hili wanaona aibu.Tulisema mapema uongozi wa simba wa sasa chini ya Mama muadilifu Barabara haubatishi na wataumbuka wengi huu ni mwanzo tu πŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ’ͺ

    ReplyDelete
  3. Kwani wao utopolo wachezaji wazawa wanatoa mil mia ngapi..au ulitaka alipwe mil 20 sawa na Kabwili?

    ReplyDelete
  4. Mmeshakamuliwa, mlitaka mumchukue bureee..hehehe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic