August 9, 2021


 IMEELEZWA kuwa mshambuliaji wa Simba, Chris Mugalu yupo kwenye rada za Klabu ya RS Berkane ya Morocco ambayo inafundishwa na Kocha Mkuu, Florent Ibenge.

Ibenge anamtambua Mugalu kwa kuwa alikutana naye kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wakati ule anaifundisha AS Vita ya Congo.

Kwenye mchezo wa hatua ya makundi walipokutana Congo, Mugalu aliyeyusha furaha ya AS Vita kwa kufunga bao kwa penalti na aliwasumbua mabeki wa timu hiyo jambo ambalo limemfanya akubali uwezo wake.

 Ikiwa mambo yatakwenda sawa huenda dili hilo likamiliziwa nchini Morocco kwa kuwa Klabu ya Simba imepanga kwenda huko kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa 2021/22.

8 COMMENTS:

  1. Haendi popote story tu,kumbe mikia baada ya kusajili Banda wamemaliza idadi? 10 tayari mnatakiwa kupunguza watu hili msajili , mwisho wa ngebe.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Subiri inyeshe tuone panapovuja. Simba wana uwezo wa kuvunja mkataba na mchezaji watakae hisi haendani na kasi yao na kumsajili mchezaji mwengine we upotolo acha mchecheto.

      Delete
  2. Sasa Kama simba wataamua kuuza wachezaji wao wanaotakiwa na vilabu mbali mabali Africa watabakiwa na Wachezaji kweli.?

    ReplyDelete
  3. Wachezaji gani wanatakiwa issue hapa Ni papara za Usajili,mliwajaza na ukiangalia wote Ni foreigners na hata kwenye Ligi walikuwa Wanacheza Saba au nane Sasa wenzenu wanajaza nafasi mnaanza oh wacheza Ndomboro mnadhani hatuwajui,mwambie KARIA mbadili kanuni iwe Kama ya CAF na Corona ndipo mtapata nafuhu,ninyi hapa dili kwenu Ni wa ndani tu ,nao mnakuwa Kama mnacheza kamali cse wa mwaka Jana Ni BOCCO,KAPOMBE,SHABALALA
    na Manula hata DILUNGA ,waliobaki mna gamble cse mtakao waleta na hao sawasawa .

    ReplyDelete
  4. Mnavunja benki kwa nyundo ?tajiri kaumbuliwa na Manara yupo hoi ,yetu macho tu.

    ReplyDelete
  5. Hii ndio maana ya kuwa na Technical bench lenye kujielewa.Hakuna maana ya kusajili lundo la wachezaji wapya wakati kuna dirisha dogo la usajili mwezi wa December.Huu ni mwezi wa August na mashindano CAFCL yanaanza Sept,10/11 then unaanza lini pre-season training?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mie nawapa pongenzi Viongozi wa Simba kama kweli wamezingatia ripoti ya benchi la ufundi.Vilabu hivi vitatu vikubwa vimekuwa zinasajili kila dirisha kubwa lundo la wachezaji wapya kama fasheni show ya warembo inayofanywa kila mwaka.Upigaji wa cha juu bado zinawasumbua hivi vilabu.

      Delete
  6. Utopolo hawana akili hiyo yak kufikiri kuwa Kuna dirisha dogo la usajili. Usajili wao ukichemka inabidi wabakie na akina Sarpong wengine mpaka mwisho wa msimu. Matokeo Wana lalamikia TFF.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic