August 30, 2021


 BAADA ya kumaliza maandalizi ya kwanza kuelekea msimu mpya wa 2021/22 na kurejea Tanzania, kiungo  wa Simba Peter Banda ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Malawi.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes iliweka kambi kwa muda nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.

Banda ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Malawi kwa ajili ya kujiandaa na michezo ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka 2022. 

Pia wapo nyota wengine wa Simba ambao wapo kwenye kambi ya timu ya taifa ya Tanzania ambao ni pamoja na Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein pamoja na John Bocco.


1 COMMENTS:

  1. Banda ni mchezaji mazuri na simba wamesajili vizuri ila katika wachezaji kama wanasimba tuliwapigia kelele Sana wasajiliwe mapema tu Basi ni Moses Phiri wa zanaco sijui tatizo lilikuwa wapi nadhani hata umri wake ni mdogo na kama sikosei ni mfungaji bora wa ligi ya zambia. Yule mwanamdogo ni mpambanaji Kama shabiki wa Simba nisingependa kuona asajiliwe na timu yeyote nchini itakuwa shida.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic