August 31, 2021

 


MAKAMU Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela leo Agosti 31, 2021 amemtangaza, Senzo Mbatha kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu (C.E.O) wa Klabu hiyo.

Kwa majukumu hayo ana jukumu la kusimamia mchakato wa mabadiliko kufikia mwisho na aliyekuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Klabu hiyo, Hajji Mfikirwa atakuwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala.


Fredrick Mwakalebela ametangaza hayo baada ya Katiba ya Yanga kubadilishwa baada ya wanachama wa Klabu hiyo kupitisha mchakato wa mabadiliko kwa asimia mia.


Mbata awali alikuwa mshauri mkuu wa Yanga kuelekea kwenye mabadiliko baada ya kubwaga manyanga ndani ya Simba ambapo alikuwa kwenye nafasi hiyo.

Ndani ya Yanga anakuwa ni Mtendaji Mkuu wa mpito, (Interm CEO) wa Klabu ya Yanga kufuatia utekelezwaji wa mfumo wa uendeshaji wa klabu.

8 COMMENTS:

  1. Bravooo! Jitu litakufa!

    ReplyDelete
  2. Tanzania ni nchi yenye amani, tafadhali sana tusijenge chuki na uhasama baina ya vilabu vyetu

    ReplyDelete
  3. Jitu lilishakufa 2-1juzi tar 29 mbele ya umati wa mashabiki wake

    ReplyDelete
  4. Badala ya kutukanana, lkuumbuwana na kukomowana, viongozi na mashabiki ni vema wazishugulikie m maendeleo ya timu zao. Yaliyokuwepo hivi sasa ni majaribio yaliopo sasa ni kuangushana na pindi yakitokea hayo moja ya timu kubwa ikianguka, tujuwe hamasa ya mpira itatoweka kwani hamasa iliyokuwepo sasa ni kuwepo kwa hizi tibu kubwa zinapopambana la sio kila kitu kitageuka. Tujisahihise kabla hayajstufika. Yaliyojengwa kwa miaka mua yanabomoleka kwa siku chini ya mia na tumlani bilisi

    ReplyDelete
  5. CEO ni WA kampuni sio klabu kampuni iko wapi sasa imesajiliwa?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic