August 3, 2021

 SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeingia mkataba wa haki ya matangazo ya Ligi Kuu kwa upande wa Radio na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wenye thamani ya Sh bilioni 3.

Mkataba huo ambao umesainiwa leo Agosti 3,2021 ni  wa muda wa miaka 10.


Mkataba huo umesainiwa baada ya kuwa na makubaliano kwa pande zote mbili ambapo Rais wa TFF, Wallace Karia aliweza kumwaga wino kwa ajili ya mkataba huo kwa upande wa TFF.

Ni Gabriel Nderumaki, Mratibu wa Masuala ya Masoko alikuwa ni mmoja ya wale waliosaini mkataba huo kwa upande wa TBC.

Karia amesema kuwa ni hatua nzuri ambayo wamefikia katika kusaini mkataba huo ambao utaongeza thamani ya soka la Tanzania pamoja na ubora wa ligi.

5 COMMENTS:

  1. TBC wachovu wamelamba mkataba, hongera.

    ReplyDelete
  2. Watatumia hela za werikali (OC) kulipia gharama za huo mkataba? Maana sioni wakijiendesha hawa kazi yao kubwa siasa na propaganda.

    ReplyDelete
  3. Radio nyengine marufuku kutangaza au

    ReplyDelete
  4. Ahahahahah,
    Yaan TBC1 ubunifu wao umeishia kwenye matangazo ya redio, hata ZBC wanaafadhali ktk masuala ya michezo lkn TBC1 hawana maajabu

    ReplyDelete
  5. Wameanza kutangaza mpira miaka yakina Charles Hilary mpka leo lkn hakuna ubora ikilinganisha na ukubwa wa TBC1

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic