August 3, 2021


 IMEELEZWA kuwa Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes ana ofa nne mkononi kutoka kwa timu tofauti ambazo zinahitaji kupata saini yake.

Sababu kubwa ya Gomes kuwa kwenye rada katika timu tofauti ni ubora wake ambao ameweza kuonyesha akiwa na kikosi hicho ikiwa ni msimu wake wa kwanza baada ya kurithi mikoba ya Sven Vandenbroeck.

Miongoni mwa timu ambazo zinahitaji saini yake ni pamoja na Raja Casablanca ya Morocco, Mamelod Sundowns pamoja na timu nyingine kutoka Misri.

Kwa sasa Gomes yupo zake nchini Ufaransa kwa ajili ya mapumziko baada ya ligi kuisha na ni Septemba 25 mechi ya ufunguzi ya Ngao ya Jamii inatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa ambapo itakuwa ni Simba v Yanga.

Habari zimeeleza kuwa kabla ya kusepa Bongo alikutana na Mohamed Dewji ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya  Wakurugenzi ndani ya Simba.

"Kabla ya Gomes kusepa Bongo alikutana na Mo na kufanya naye mazungumzo, walizungumza pia kuhusu mkataba wake ambapo aliweka wazi kwamba alikuwa na ofa kutoka timu mbalimbali.

"Kutokana na utendaji wake kazi mzuri walikubaliana kumuongezea mkataba hivyo bado yupo kwa kuwa alisaini dili la mwaka mmoja," ilieleza taarifa hiyo.

Julai 30, Mo aliongea na Waandishi wa Habari katika Ukumbi uliopo ndani ya Hotel ya Golden Jubilee na aliweka wazi kwamba amekuwa akitumia gharama kubwa kwa ajili ya usajili wa Simba ikiwa ni pamoja na kuwaleta makocha na yote hayo yanatokana na mapenzi ya timu hiyo tangu akiwa mdogo.


2 COMMENTS:

  1. Huyo si kocha aliyetimuliwa kwengineko wengine wakaona uhondo labda kwa bei chee wakampkea kwa mikono miwili na ndio mana tunaona Gomes anatakiwa kila pembe kama alivo Sven kwa sababu Sinba instuluza akili inapotaguta wachezaji wa nje ns wa ndani

    ReplyDelete
  2. Kichwa cha habari timu 4 kwenye maelezo timu mbili ya 3 haikutanjwa..hehehe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic