August 17, 2021


 KUNA kila dalili straika wa Yanga, Waziri Junior akatimka ndani ya Yanga baada ya timu kibao kutaka kumnunua na zingine zikimtaka kwa mkopo wa mwaka mmoja.

 

Waziri amekosa nafasi ya kucheza ndani ya Yanga tangu aliposajiliwa kutoka Mbao FC msimu uliopita na hata alipokuwa anapewa nafasi ya kucheza amekuwa haonyeshi kile mashabiki walichokuwa wanatarajia.

 

Taarifa kutoka Yanga zinasema Polisi Tanzania, Mtibwa Sugar, Dodoma Jiji na Kagera Sugar wanekuwa wakipishana kwenye ofisi za Yanga wakitaka huduma ya straika huyo ambaye amefunga mabao mawili kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

 

Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga Thabit Kandoro, aliliambia Championi Jumatatu kuwa Waziri ameletewa ofa nyingi sana kiasi ambacho wameamua kumtuliza asiende Morocco kwenye kambi ili viongozi waamue kama watamuuza au atabaki.

 

“Kiukweli kuna timu nyingi sana zinamuhitaji Waziri ingawa sisi bado hatujaamua kama tutamuuza au atabaki, ndiyo maana kwa sasa tumeamua asiende kwanza kambini Morocco ili tuamue,” alisema Kandoro.

 

Yanga waliondoka jana kwenda Morocco kwa ajili ya kambi kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu na mashindano ya kimataifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic