SASA imekuwa kawaida, tumerudi kulekule kwa mwanzo. Ninawazungumzia wachezaji wetu ambao wakiwa wanaenda kutafuta maisha nje ya nchi wanatuachia matumaini tele kuwa wanaenda kuitangaza nchi kuwa kwetu kuna vipaji lakini haizidi mwaka kama siyo miezi sita utashangaa wanarudi.
Ni wachache ambao wanavumilia mengi na kupambana lakini wachache wanashindwa na kuamua kurejea nyumbani. Wapo ambao soka linawashinda na wengine kutokana na sababu zao binafsi.
Mbwana Samatta ambaye kwa sasa anakipiga Fenebarche ya Uturuki ni mfano bora na role model kwa wachezaji wengi wazawa kwa sasa na ukiangalia amevumilia mengi hadi amefika hapo alipo.
Aliwahamasisha wengi sana baada ya kutua Genk ya Ubelgiji kisha Aston Villa ya England. Vijana wengi walipambana na kupata nafasi nyingi za kwenda kufanya majaribio na wengine kuanzia vikosi vya vijana.
Lakini hilo rundo pia ni kama linapukutika na kuanza kurejea nyumbani mmoja mmoja, hivi ni kwamba vijana wetu hawawezi kuvumilia au ni nini.
Mchezaji wa zamani wa Yanga, Maka Edward mwaka 2019 alijiunga na timu ya Morocco ya Moghreb Athletic de Tetouan ambapo alisaini mkataba wa miaka minne ambapo aliitumikia kwa miaka miwili na sasa amerudi anapambana kwenye ndondo huko.
Championi lilipomuuliza kama yuko mapumziko na atarudi kwenye klabu yake akasema harudi kwa kuwa ameshindwa maisha ya huko. Alisema hana tena hamu ya kwenda nje kucheza kwa sasa kwani anaona anapoteza muda wake.
Lakini hapo aligusia pia visa kuwa jamaa walisema watamtumia visa baada ya ile ya awali kuisha lakini hawakufanya hivyo, hapohapo anasema kati ya vitu vilivyomkwamisha ni lugha ndio ilikuwa tatizo kubwa sambamba na ugumu wa ligi ambayo alikuwa akicheza ile ya U21 na kikosi cha wakubwa aliishia kukaa benchi.
Hapohapo Nickson Kibabage aliyekuwa DifaĆ¢ El Jadida ya Morocco baadaye Berrechid na sasa inadaiwa amerejea nchini baada ya kuachana na timu yake.
Wako wengi ambao wanarudi kimyakimya baada ya kushindwa kama sio kuvumilia basi kushindwa kabisa maisha ya huko nje. Leo hii klabu kubwa zinakuja Tanzania kusajili wachezaji wa kimataifa na sio wazawa.
Mastaa kama Clatous Chama aliyekuwa Simba, Tuisila Kisinda wanasajiliwa kwa fedha nyingi na RS Berkane ya Morocco huku Luis Miquissone naye akitua Al Ahly ya Misri.
Hivi wachezaji wetu hawaoni wivu. Mtu anasajiliwa kutoka nje ya nchi anakuja hapa unacheza naye halafu anasajiliwa tena nje ya nchi kwa fedha nyingi, ninyi hamuoni wivu au ni kuridhika kucheza Simba na Yanga?
Wachezaji wengi tu wamerudi nchini kama Habibu Kyombo, Yahya Zayd, Farid Musa, Eliud Ambokile, Ramadhan Singano hawa ni kati ya wengi waliowahi kwenda nje na wakarudi kwa vipindi tofautitofauti.
Labda tuwatafute na hao wengine watuambie kule nje kuna nini, mbona hawadumu kama kaka yao Samatta na Simon Msuva?
Hapa pamoja na Wachezaji tuwe wa kweli,Makocha wa Soka,Waandishi na Watangazaji wa Michezo lenu moja hata nyie mule mule Kiswahili kimewaoa .hamtoki????
ReplyDeleteTumeona hata AzAM. Kuna Channel Mtangazaji Muganda/Mkenya lkn wenzetu mmeng'ang'ania FM Redio na Eng/Swahili utasikia mala assist,striker ,semi bending ball,mbona hatuwasikii nje ,mnakimbilia habari na vyombo vya Kiswahili.
ReplyDelete