August 24, 2021

 


YANGA imefanya umafia huko nchini Morocco baada ya kudukua mtandaoni linki ya mchezo wa kirafiki wa Simba na kuungalia wote, huku wakisema mabao hayakuwa halali.

 

Simba Jumamosi ilicheza mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu dhidi ya AS Rabbat ya nchini Morocco ambako timu hiyo imeweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na msimu ujao na kumaliza kwa sare ya mabao 2-2, huku mabao ya Simba yakifungwa na Ousmane Sakho na Hassani Dilunga.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatatu, wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa timu hiyo waliutazama mchezo wote pamoja na kwamba ulipigwa pini usionyeshwe.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, walipanga kuwatuma mashushushu kwenda kuutazama mchezo  huo, lakini kutokana na umbali wa mji ambao Simba wamefikia huko Rabbat, walishindwa lakini wakawatumia watu wa pale pale kuwapa linki.

 

Aliongeza kuwa kutoka Marrakech ambako wamefikia kwenda Rabbat ni mwendo wa saa nane kwa kutumia gari, hivyo wakawatumia wataalam wao mitandao kwa ajili ya kudukua linki ya mchezo huo ambao ulikuwa ukionyeshwa mtandaoni kwenye mji husika tu.

 

“Tulipanga muda mrefu kwenda kuwatazama Simba wakicheza mchezo wake wa kirafiki kwa lengo kuwajua wachezaji wapya waliowasajili pamoja na kuujua ubora wa timu yao.

 

“Lakini ilishindikana kutokana na umbali uliopo kutoka katika mji tuliokuwa ambao Marrakech kwenda Rabbat hapa Morocco walipofikia Simba.

 

“Licha ya kushindwa kwenda huko, lakini tumefanikiwa malengo yetu baada ya kocha na wachezaji kufanikiwa kuwaangalia Simba kwa kupitia mtandaoni, baada ya kuidukua linki ya mchezo huo.

 

“Kocha ameona ubora na upungufu wao, na kikubwa Simba wenyewe mabao yenyewe ambayo wamefunga yote yalikuwa ya kuotea (offside),” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Akithibitisha hilo Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela alisema kuwa “Tumeuona mchezo wa kirafiki ambao Simba wameucheza kupitia mtandaoni, hivyo tumeona upungufu na ubora wao, kikubwa tukutane katika msimu ujao ambao tumepanga kufanya mengi makubwa.”

 

Taarifa zinasema kuwa wakati mchezo unaendelea kuna mtu wa upande wa Yanga alikuwa pale uwanjani na ndiye alifanya kazi kubwa hakikikisha mechi wanaiona.

14 COMMENTS:

  1. Mafanikio ya time ndogo ndiyo kama haya. Aibu iliyoje kujisifia ujingaa huu badala ya kuandaa timu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tena ni ujinga wa hali ya juu! Na mpumbavu mwingine mpaka akajivisha u-referee, eti magoli yalikuwa ya off-side! Akili gani hizi jamani! Yule kocha wao wa zamani aliyewaita yale majina fulani fulani kweli hakukosea!

      Delete
  2. Inferiority complex itawaua Utopolo. Kila siku kutafuta kiki.Wasiwasi wa nini?Si wamesajili sasa mchecheto wa nini?

    ReplyDelete
  3. Kama hiki ni cha kweli basi mtanisamehe sana, yanga ni wapumbavu. Utapitezaje muda na resources kwa ujinga huu? Kumbe hata frienly match za simba zinawatesa hadi kulalamika magoli sio ya haki ili hali waliofungwa magoli hayo wala hawana habari? Duh! Aibu.

    ReplyDelete
  4. Mimi nahisi mwandishi amedhamiria kuwadhalilisha utopolo kijanja, hawewezi kuwa wajinga kiasi hiki hadi kujidhalilisha namna hii

    ReplyDelete
    Replies
    1. Uko sahihi ndugu hii ni kazi ya mwandishi salehjembe na usimba wake ndio unaomsumbua.

      Delete
  5. Hata kama ni kweli kuna haja gani ya kunigamba hadharani, ni sawa na mpiga chabo atangaze ujinga wake wenye akili na maadili watamwona punguani tuu hata kama akili yake imemdanganya kapata faida

    ReplyDelete
  6. Acheni kutoka povu mnachezewa akili zenu nanyi bila kufiri kwakina mnatoka povu kirahis "brainstorm your self"

    ReplyDelete
  7. Kusema kweli viongozi Yanga mnazidi kutufedhehesha. Pre season zero. Sasa mnaingiza na iwendawazimu. Ati mmewasoma wao wako katika kupanga kikosi chao ndio maana mamefanya sub kibao. Baada sisi kushughulika na kikosi chetu mnatutia aibu nyinyi sio weledi

    ReplyDelete
  8. Hivi ninyi mnao comment humu ,kweli hata Kama Ni michezo huwa mnakwenda Ibadani,(bila kujali dini au dhehebu)?mnajua maana ya kudhania,kusingizia au mnakumbuka Kwanini juzi pamekuwa na mtafaruku Gazeti la Uhuru na Rais wetu wa Nchi,nadhani pamoja na utani siyo kila habari maadam,ipo upande usiyo penda ikikukela hata Kama imetungwa utukane watu ,takeni vinywa vyenu na ndimi zenu zitoe maneno yakujenga,yanayopendeza mbele ya Watu,.Naamini hata Wanaocheza Mpira uomba Mungu/Mola ,siyo kila Comment utukane au hata Kama mtu hajui mshauri siyo kejeli na matusi.Hivi ukweli kwa Mpira wa Kisasa Kuna haja ya kupata taarifa za mechi Tena pre season kwa kujificha,na vile vile kwa Utandawazi uliopo unaweza kucheza mechi ukaificha????hususani yenye interest na Watu ,nawasihi acheni kupandisha munkali.Jamani tumeona Timu zote Duniani pre season kila kitu wazi Leo eti Timu inajificha .Hii kwa ki Lugha tunasema unachoma Nyumba unaficha moshi.Nimewapenda Wazee wa mabadiliko mna Moto Sana vijana wa Mbumbumbu kifupi mnabore.

    ReplyDelete
  9. Sawa lkn haitakusaidia wawe ?Mavi au mikojo haitakusaidia.Zaidi ya kufanya uishi na kuwa mtu wa hivyo na zaidi hata kizazi chako(wanao) utawarithisha tu.

    ReplyDelete
  10. Daah!! Utopolo wana safar ndefu sana mpk wamfikie mnyama

    ReplyDelete
  11. This is uto akili za kiuto na mafanikio ya kiuto

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic