UONGOZI wa Coastal Union umeweka wazi kuwa kwa sasa upo kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2021/22.
Ofisa Habari wa Coastal Union, Miraji Wandi ameweka wazi kuwa kila kitu kinakwenda sawa na wanaamini kwamba watafanya vizuri kwa msimu ujao.
"Tumejipanga vizuri kwa ajili ya msimu ujao na tunahitaji kuona kwamba matokeo ambayo tutapata yatakuwa ni mazuri kwetu.
"Kikubwa ni kuona kwamba tunamaliza msimu katika nafasi nzuri hatuhitaji kuona timu inakuwa kwenye presha ya kutaka kushuka daraja," amesema.
Msimu wa 2020/21 timu hiyo iliweza kucheza play off na timu ya Pamba FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza na iliweza kushinda jambo ambalo limeifanya iwe na uhakika wa kubaki ndani ya ligi msimu ujao.
Haikuwa kwenye mwendo mzuri kwa kile ambacho Juma Mgunda aliyekuwa Kocha Mkuu zama hizo kwa sasa ni Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi kwa kueleza kuwa waliwakosa nyota wao muhimu katika kikosi hicho ikiwa ni pamoja na Bakari Mwamnyeto ambaye aliibukia Yanga pamoja na Ibrahim Ame ambaye aliibukia Simba.
Usajili ambao wameufanya kwa sasa ni pamoja na ule wa Kocha Mkuu ambapo wanaye Melis Medo raia wa Marekani pia kipa ni yule Mussa Mbissa ambaye alikuwa ndani ya Mwadui FC.
Jana Septemba 9 timu hiyo ilicheza mchezo wa ndani na Simba kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya na ngoma ilikuwa 0-0.
Undumila kuwili unawaponza ,mkicheza na Simba utadhani Timu ya daraja la nne,msipoacha mtashuka mnalea mishipa.
ReplyDelete