September 3, 2021


 KLABU ya Manchester United imemkabidhi rasmi jezi namba 7 nyota Cristiano Ronaldo ambaye amesajiliwa hivi karibuni.

Namba 7 ilikuwa inavaliwa na mshambuliaji Edison Cavani ambaye amepewa namba 21 ambayo awali ilikuwa inavaliwa na Daniel James ambaye ameuzwa kwenda Leeds United.


Ronaldo amemshukuru Cavani kwa kukubali kumpa jezi hiyo ambayo ina historia kubwa kwa mchezaji huyo.


"Sikutarajia kuwa itawezekana kuvaa tena namba 7, namshukuru sana Cavani kwa ukaribisho huu murua," amesema.


Nyota huyo alikuwa alikuwa anakipiga ndani ya Juventus na amerejea hapo baada ya miaka 12 kuyeyuka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic