September 3, 2021

 


MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Mayele, amewatuliza mashabiki wa timu hiyo kwa kutoa kauli nzito iliyoendana namatarajio ya kuipa mafanikio makubwa timu hiyo.

 

Mayele ni ingizo jipya ndani ya Yanga ambapo amesajiliwa akitokea AS Vita ya nchini DR Congo.


Mshambuliaji huyo wikiendi iliyopita kwenye Kilele cha Wiki ya Mwananchi, alicheza mechi ya kirafiki dhidi ya
Zanaco iliyomalizika kwa Yanga kufungwa 1-2.


Akizungumza na Spoti Xtra, Mayele alisema: “Mashabiki zetu wanatakiwa kuwa wavumilivu kwa sasa kwani ndio kwanza tunaanza, timu bado inaandaliwa vizuri na mwalimu, tunaamini kila kitu kitakuwa sawa.
“Sisi kama wachezaji bado tunaendelea kupambana kwa ajili ya kufanya vizuri msimu ujao.

 

Tunataka kuifikisha timu kwenye malengo. Wasubiri waone.“Hakuna ambaye anapenda kuona timu inafanya vibaya, kama ambavyo mashabiki wanaumia pale matokeo yanavyokuwa mabaya basi na sisi wachezaji tunaumia, hivyo hatutakubali hilo litokee.

2 COMMENTS:

  1. Tulieni dawa iwaingie

    ReplyDelete
  2. Nashauri maneno yapu gue badala yake wapige kazi. Maneno mengi ni dalili ya kutojiamini

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic