September 29, 2021

 



LEO Septemba 29, Ligi Kuu Bara inaendelea ambapo ni mzunguko wa kwanza kwa timu kuingia uwanjani kusaka pointi tatu muhimu.

Mabingwa watetezi wa taji la Ligi Kuu Bara ni Simba ambao walitwaa msimu uliopita na walianza jana kusaka ushindi mbele ya Biashara United, Uwanja wa Karume na ngoma ilikuwa Biashara United 0-0 Simba.

Kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi baada ya kutwaa Ngao ya Jamii Septemba 25 kiliposhinda bao 1-0 mbele ya Simba leo saa 10:00 jioni wanaanza mbio za kulisaka taji la 28 la Ligi kuu Tanzania bara kwa kucheza na Kagera Sugar katika Uwanja wa Kaitaba.


Pia saa 8:00 mchana Polisi Tanzania wao watamenyana na KMC katika mchezo wa kwanza kwa timu hizo. Mechi zote zitakuwa mubashara Azam TV.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic