BREAKING:MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Klabu ya Simba, Mohamed Dewji ameamua kukaa pembeni kwenye nafasi hiyo kutokana na makubaliano ya Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Simba.
Taarifa ambayo ameituma Mo amesema kuwa:"Miaka minne tumepata mafanikio makubwa,tumeshinda ligi mara nne kufanya vizuri Champion League,(Ligi ya Mabingwa Afrika).
"Bado ninaipenda Simba. Tumefanya mkutano wa bodi tarehe 21,9,2021 tumekubaliana kwamba mimi nitastep down, (kuwa pembeni) kuwa chairman (mwenyekiti) Simba SC.
"Ninaomba wanachama wa Simba msifikirie mimi ninaondoka kwenye Simba, mimi bado ni mwanahisa, ninaipenda Simba, tumekubaliana kufanya hivyo kwa sababu mimi nimekuwa ninasafiri sana," .
Daaa kaz ipo
ReplyDeleteMo anahela ila Salum be Try again yupo vizuri Zaidi kiungozi kwa hivyo hakuja haribika kitu.
DeleteAtuambie kwanza akina Chama na Miquissone wameuzwa shilingi ngapi na Fedha za mauzo zipo Akaunti ipi?
DeleteMAJUKUMU NI MENGI, MALI ZA FAMILIA, HUKU TIMU, UNADHANI KAZI NYEPESI?
ReplyDeleteKwani miaka yote minne alikuwa hayo majukumu nani alikuwa anayafanya?
DeleteMo Dewji ni tajiri wa kweli. Kama unamuuza Chama na Kondeboy ukarudisha pesa yako kidogo kwa nini uendelee kupata hasara tena? Unalipa kocha, wachezaji na kila kitu bado marefa, uchawi na mambo kibao faida utapata lini? Ameonyesha uwezo wake wa kufikiri na kwa nini yeye ni tajiri." Tafakari na chukua hatua"
ReplyDeleteAmesoma alama za nyakati. Maana mayai viza na maneno ya shombo vinafuatia sasa maana ufalme wa simba umefika kikomo
ReplyDeleteha ha ha ha ha, kachomoa betri huyo hana lolote miaka yote minne alikuwa hasafiri???
ReplyDeleteMmmmh kusafiriiii??????👀👀👀
ReplyDelete