September 24, 2021


 MASTAA wa Simba hivi karibuni walipelekwa Hospitali ya Muhimbili ya jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya moyo kabla ya mchezo wa Kariakoo Dabi.

 

Baadhi ya mastaa wa Simba ni Sadio Kanoute, Denis Kibu, Ousmane Sakho, Peter Michael na Henock Baka waliojiunga na timu hiyo hivi karibuni.

 

Simba na Yanga zinatarajiwa kujitupa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam kuvaana katika mchezo wa Ngao ya Jamii utakaopigwa Jumamosi hii.

 

Akizungumza na Championi JumatanoKaimu Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema kuwa huo ni utaratibu wa kawaida kwa wachezaji wao kufanyiwa vipimo vya moyo kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Bara.

 

Kamwaga alisema upo umuhimu mkubwa wa wachezaji wao kufanyiwa vipimo vya afya ikiwemo moyo ambao ni ugonjwa hatarishi kwa wachezaji.

 

Aliongeza kuwa, vipimo hivyo viliwahusisha wachezaji wote wapya na wa zamani pamoja na benchi la ufundi ili kujua afya zao.

 

“Kama Simba timu kubwa sisi tumekuwa na utaratibu wa kuangalia afya za wachezaji wetu kwa kuwafanyia kipimo cha ugonjwa wa moyo.

 

“Hivyo asubuhi wachezaji na benchi la ufundi wote walifanyiwa vipimo vya ugonjwa wa moyo katika Hospitali ya Muhimbili.

 

“Ugonjwa wa moyo unajulikana jinsi ulivyo hatarishi kwa wanamichezo, hivyo tumeona kuwafanyiwa mapema vipimo kabla ya kuanza kwa ligi,” alisema Kamwaga.

6 COMMENTS:

  1. Hii nimependa Sana Simba pongezi kwenu.Tanzani ungekuwa utaratibu kwa timu zote za ligi kuu ingependeza zaidi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Upo sahihi kbs ndugu yangu, ni utaratibu mzuri sana.

      Delete
  2. Wengine igeni kama kawaida ijapo siri siri

    ReplyDelete
  3. Wengine wanafanya HIVYO Kabla ya kumsajili mchezaji .. je ukikuta ana Tatizo utafanyaje?

    ReplyDelete
  4. Tatizo linaweza kutokea wakati wowote. Unaweza kumpeleka akapimwe na akapata matatizo baadaye na vice versa.Lakini ni jambo zuri kupima. Ericsson alipimwa kabla na kidogo afe.Ni jambo la kuigwa na timu zote.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hakika TFF WALIWEKEE SHERIA IWE KWA TIMU ZOTE ILI WASIJE WAKAFA WACHEZAJI WETU ! MAANA WENGINE WANACHEZA JUDO!
      pia TFF ninaishangaa SANA kwa nini wakati mwingine wasitumie HEKIMA???
      KWA MFANO JOHN Rafael BOCCO ALIUMIZWA KWA MAKUSUDI NA MCHEZAJI MUKOKO TUNOMBE SASA MUKOKO TUNOMBE ANILIPA FAINI PESA INAENDA KWA TFF KWA KIDONDA KIPI ????

      BY KOMANDOO WA YESU

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic