September 24, 2021


 KOCHA Mkuu wa Simba, Mfaransa, Didier Gomes ni kama amewamaliza watani wake wa jadi, Yanga, ni baada ya kuzinasa video za michezo miwili waliyoicheza sawa na dakika 180.

Timu hizo zinatarajiwa kuvaana kesho Jumamosi saa 11:00 jioni katika mchezo wa Ngao ya Jamii utakaopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar.


Katika mchezo huo, kila timu itaingia uwanjani ikiwa na mabadiliko ya kikosi chake baada ya kufanya usajili katika kuelekea msimu ujao kama ilivyo kwa Yanga ambapo kuna mshambuliaji wao tegemeo, Heritier Makambo.


Mmoja wa mabosi wa Simba kutoka ndani ya Benchi la Ufundi la timu hiyo, ameliambia Championi Jumatano, Gomes ameomba michezo miwili waliyoicheza wa Wiki ya Mwananchi waliyocheza dhidi ya Zanaco ya Zambia pamoja na ule wa kimataifa dhidi ya Rivers United uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa.


 Bosi huyo alisema kuwa, kocha anatarajiwa kukaa kikao na mtathmini viwango, Culvin Mavhunga kutoka nchini Zimbabwe ambaye alitoa mchango mkubwa kwa timu hiyo katika msimu uliopita.

Aliongeza kuwa mara baada ya kocha huyo kukaa kikao na Mzimbabwe, haraka atakutana na wachezaji wake jioni kwa ajili ya kuangalia video hizo na kikubwa kuangalia upungufu na uimara wa Yanga mpya.


“Kocha Gomes amekuwa na utaratibu wa kuangalia video za mechi za wapinzani walizozicheza kabla ya kukutana nao uwanjani.

“Tayari kocha ameagiza kupatiwa video mbili za michezo iliyopita ya Yanga ambayo ameicheza na aliyepewa kazi hiyo ni mtathmini viwango vya wachezaji ambaye ni Culvin.


“Tayari video hizo amezipata ambazo Yanga wamecheza dhidi ya Zanaco na Rivers na kikubwa anataka kuona ubora wa wapinzani kwa ajili ya kuangalia viwango vyao,” alisema bosi huyo.


Akizungumzia hilo, Kaimu Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema kuwa: “Hilo suala la benchi la ufundi na kingine nikizungumzia ninakua kama ninatoa siri za kambi, kikubwa timu inaendelea na maandalizi ya mchezo huo.”

10 COMMENTS:

  1. Mambo safi kwanza subirs kimbunga baadae

    ReplyDelete
  2. Sio rahisi hivyo.Simba inabidi wawe na video za akina Aucho na na juma shabani ambao hawakuwemo kwenye ligi ya mabingwa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hapo wanapotea kwani hizo mechi Aucho, Djuma na Mayele hawakuwepo na hajui muunganiko wao umeandaliwa vipi. Hehehe..jitu litakufa!

      Delete
    2. Udhaifu wa Dickson Job na Mwamnyeto unatosha kuutumia

      Delete
    3. Kama walikua na timu pre season na wakamshindwa zanaco,acha kujitia matumain tena inawezekana wakaisababishia timu ikafungwa.

      Delete
    4. Kocha ANAUSOMA MFUMO NA MUUNGANIKO TARAJIWA NDIO MAANA YA KUSOMEA UKOCHA

      Delete
  3. Unabii unasema simba itamiliki mpira kama ilivyo jadi na kawaida yao,goli atafunga banda,bocco na asmane sakho,zitakazo kula miamba kama zote

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hiyo Ni nzuri Sifa kwa YESU!
      By Komandoo wa Yesu

      Delete
  4. Umiliki ni 60 kwa 40

    ReplyDelete
  5. Kelele nyingi tusubirie uwanjani,huko kuweweseka tu,Naipenda yanga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic