September 19, 2021


 

VIVIER Bahati, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa mchezo wao wa jana wapinzani wao walibadili mbinu jambo lililowafanya wapate tabu kwenye ushindi wa mabao mengi.

Wawakilishi hao wa kimataifa kwenye Kombe la Shirikisho jana waliweza kushinda bao 1-0 dhidi ya wapinzani wao Horseed FC ya Somalia na kuweza kusonga hatua nyingine kwa kuwa mchezo wa kwanza walishinda kwa mabao 3-1.

Akizungumza na Saleh Jembe, Bahati amesema kuwa walitambua kwamba mchezo wao ungekuwa mgumu jambo ambalo liliwafanya wawape somo la kujiamini wachezaji wao.

"Mchezo wa kwanza tulishinda kwa mabao mengi ilikuwa ni furaha kwetu lakini mchezo wa pili mambo yamekuwa tofauti hiyo inatokana na mbinu za wapinzani wetu.

"Kikubwa tuliwaambia wachezaji kwamba wapambane kazi haitakuwa nyepesi na wao wamefanya hivyo mwisho wa siku tumeshinda na tumesonga mbele," .

Azam FC inasonga mbele kwa jumla ya mabao 4-1 huku bao la jana likipachikwa na kiungo wao Ismail Kada kwa shuti lililomshinda kipa wa Horseed FC.

Nyota wa mchezo ni Idd Suleman, 'Nado' ambaye alikuwa ni machachari na msumbufu muda wote alipokuwa ndani ya uwanja jambo ambalo liliwafanya Horseed FC wapoteane licha ya kucheza kwa umakini na utulivu mkubwa, Uwanja wa Azam Complex.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic