BAKARI Mwamnyeto nahodha wa Yanga amesema kuwa kilichowapeleka nchini Nigeria ni kusaka ushindi jambo ambalo wanaamini kwamba litatokea.
Leo Uwanja wa Adokiye Amiesimaka Yanga itakuwa na kazi ya kusaka ushindi kwa ajili ya kupata ushindi ili kuweza kusonga mbele kwa kuwa katika mchezo wa awali uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Yanga 0-1 Rivers United.
Ikitokea bahati mbaya Yanga ikapoteza mchezo wa leo, safari yao katika kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa itakuwa imeyeyuka mazima mpaka wakati ujao ikiwa itatokea.
Kwa kuwa walipoteza mchezo wa kwanza wakiwa nyumbani basi wana kazi ya kushinda kuanzia mabao mawili kisha wao wapambane wasiruhusu bao kuokotwa kwenye nyavu zao.
Mwamnyeto ameweka wazi kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu lakini wapo tayari kwa ajili ya kuwapa furaha mashabiki pamoja na Watanzania kiujumla.
"Mchezo utakuwa mgumu lakini tupo tayari kwa ajili ya kupambana kila mmoja anahitaji kuona tunapata matokeo na hayo ni malengo yetu na inawezekana.
"Kikubwa ni kuona mashabiki wanaendelea kutuombea dua kwani sio kazi rahisi, makosa ambayo tumeyafanya kwenye mechi zetu ambazo zimepita tumeyafanyia kazi na tunaamini kila kitu kitakuwa sawa,".
Jana kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi kilifanya mazoezi ya mwisho leo Septemba 19 kina kazi ya kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa.
Labda lakini nimeota yanga imefungwa 2-0
ReplyDelete