September 19, 2021


 WAKIWA nchini Nigeria wawakilishi wa Tanzania wamekutana na masuala yasiyowapendeza ikiwa ni pamoja na majibu ya Virusi vya Corona kuchelewa kutolewa.

Yanga leo itakuwa na kibarua cha kucheza dhidi ya Rivers United ya Nigeria ikiwa ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali.

Kwa mujibu wa Maulid Kitenge ambaye yupo nchini Nigeria amesema kuwa majibu ya Corona yamechelewa kutolewa.

Kwa hali ilivyo mambo ni magumu kwa Yanga kwa kuwa ina kazi ya kusaka ushindi na mchezo ule wa awali uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Yanga 0-1 Rivers United hivyo kikosi hicho kina kazi ya kupindua meza kibabe leo.

Pia taarifa ambayo imetolewa hivi karibuni na maripota wa Azam Media wameeleza kwamba Yanga wamegomea majibu hayo kwa kuwa yametoka saa moja kabla ya mechi ya marudio.

Taarifa rasmi kutoka Yanga zimeeleza kuwa saa moja kabla ya mchezo majibu hayajatoka na hawajapewa sehemu ya kufanyia mabadilisho ya nguo.


"Hadi hivi sasa timu ya Yanga haijapewa rasmi majibu kuhusu Covid, wametupa chumba chenye giza na wachezaji wanabadilisha nguo kwenye sehemu ya benchi. Hiki ni kitu cha kushangaza tuendelee kusubiri,".

5 COMMENTS:

  1. kwani huku nyie mlifanyaje na mpaka leo wale wachezaji wao bado mnao

    ReplyDelete
    Replies
    1. Djigui Diarra
      Kibwana Shomari
      Adeyum Saleh
      Dickson Job
      Bakari Mwamnyeto
      Mukoko Tonombe
      Jesu Moloko
      Yanick Bangala
      Heritier Mkambo
      Feisal Salum
      Yacouba Songne

      Delete
  2. Hivi YANGA mnataka Chumba cha umeme wakati mnatia hasara ??.
    Kwanini hamkuenda Na Tochi ???
    Mumekosa ubunifu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic