September 1, 2021


 WAKATI Yanga ikitambulisha wachezaji wapya kwa ajili ya msimu ujao, mshambuliaji wa timu hiyo, Mghana,Michael Sarpong amejiunga na Klabu ya Al Nahda ya Saudi Arabia kwa mkataba wa miaka miwili huku akikomba mshahara wa dola 12,000 sawa Sh milioni 27 kwa mwezi.

 

Sarpong alijiunga na Yanga msimu uliopita kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Rayon Sport ya Rwanda lakini alishindwa kuisaidia Yanga kwenye eneo la ushambuliaji hali iliyopelekea kuvunjwa kwa mkataba wake wa mwaka mmoja uliobakia.

 

 Meneja wa mshambuliaji huyo, Mnyarwanda, Alex Kamanzi alisema kuwa tayari mchezaji wake ameshajiunga na Al Nahda baada ya kumalizana na Yanga kufuatia kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake.

 

“Sarpong ameshapata timu yupo Saudia Arabia amejiunga na Al Nahda kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kuachana na Yanga kufuatia kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake.

 

“Kitu kikubwa cha kushukuru upande wetu wa kuhakikisha tumepata sehemu ya mchezaji wetu kucheza kwa sababu ndiyo lilikuwa jambo la msingi kutokana na mazingira yalivyokuwa, mchezaji yupo Saudia Arabia kwa sasa ameshakamilisha kila kitu na ameanza maandalizi ya msimu,” alisema Kamanzi.


Chanzo:Championi

5 COMMENTS:

  1. Yaani kaukosa mkwanja mkubwa kutoka kwa tajiri wa namba moja wa petroli duniani aje kuvutiwa na mkwanja mrefu wa Yanga. Hii ni kali ya hali ya juu ya mwaka Hahahaaa!!!

    ReplyDelete
  2. Kaondoka bure sasa sijui hizo hasara za kuvunja mikataba itabebeshwa Yanga au GSM

    ReplyDelete
  3. Hiyo ni faida yake na huwenda ikatokea hali ya kutomuelewa baadae.

    Hata hivyo mtu anaweza asiwe na juhudi mahala fln kutokana na mipango awazayo shm nyingine

    Michael anaweza kufanya maajabu huko kuliko tz kama ilivyo kwa Namiang

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic