September 4, 2021

 


RODGERS Kola ingizo jipya ndani ya kikosi cha Azam FC limeanza kuonyesha makali yake baada ya kuifungia bao timu hiyo.

Ilikuwa jana kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Zesco United nchini Zambia wakati timu hiyo ikipasha misuli kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2021/22.

Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina iliweza kushinda mchezo huo kwa ushindi wa bao 1-0 lilipachikwa dakika ya 54.

Kocha Msaidizi wa Azam FC,Vivier Bahati amesema kuwa bado wanakazi ya kuboresha kikosi hicho ili kuweza kufanya vizuri kwenye mashindano.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic