KOCHA Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi amefunguka kuwa hana mpango wa kumhamisha Feisal Salum katika eneo la kiungo mshambuliaji kutokana na kufanya vizuri zaidi katika eneo hilo.
Feisal kabla ya kucheza katika eneo hilo alikuwa anacheza katika eneo la kiungo wa ulinzi akiwa sambamba na Mukoko Tonombe.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Nabi aliweka wazi kuwa anafurahishwa na uwezo anauonyesha Feisal katika eneo la kiungo mshambuliaji hivyo wategemee wakimuona kiungo huyo akicheza mara kwa mara katika eneo hilo.
“Feisal anafanya vizuri katika majukumu yake mapya ya kushambulia, watu watamuona sana akicheza katika eneo hilo, nadhani wengi wameona na hakuna shaka na anachokifanya kwa sasa katika sehemu anayocheza.
“Feisal nilimkuta akicheza katika eneo la ulinzi lakini kwangu niliona anafaa kucheza katika majukumu ya kushambulia zaidi.
“Hii sio mara ya kwanza kutokea katika maisha ya mpira haswa katika majukumu kubadilika kwa mchezaji, mifumo ya mwalimu hubadilisha wachezaji,” alisema kocha huyo.
Hii ndiyo nafasi yake ki uhalisia ,ukiangalia kabla ya kuja Yanga akiwa Timu ya Zanzibar hucheza nafasi hiyo.
ReplyDelete