September 14, 2021


 MSHAMULIAJI wa Azam FC, Prince Dube ambaye ni mtambo wa mabao amesharejea katika kikosi hicho akitokea nchini Afrika Kusini.

Dube ambaye ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, George Lwandamina hakuwa sehemu ya kikosi kilichocheza katika mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Horseed FC hatua ya awali.

Msimu uliopita ndani ya Ligi Kuu Bara alitupia mabao 14 akiwa ni namba moja kwa Azam FC ila kukaa kwake nje ya uwanja kwa muda mrefu kuliyeyusha ndoto zake za kuwa mfungaji bora.

Katika mchezo huo Azam FC iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 jambo ambalo linawapa nafasi kubwa ya kusonga mbele licha ya kwamba bado kuna dakika 90 za maamuzi kwenye mchezo huo.

Alirejea Tanzania Jumatatu, Septemba 13 alfajiri akitokea kwenye matibabu jijini Cape Town, Afrika Kusini.


Dube amefanyiwa upasuaji mdogo, utakaomfanya akae nje ya uwanja kwa muda wa wiki sita hivyo ataukosa pia mchezo wa marudio unaoatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex, Septemba 18.

4 COMMENTS:

  1. Aliyemtafuta Prince Dube anastahili Pongezi KUBWA SANA.

    ReplyDelete
  2. Ila Prince Dube ataweza kufanya VEMA ZAIDI AKIIBGIA SIMBA YA SASA

    ReplyDelete
  3. Prince Dube akiingia SIMBA ya sasa aweza kufanya Vema zaidi Na zaidi

    ReplyDelete
  4. Dube mwamba sana Mungu amponye haraka Ili aendelee na kuwakera namkubali sana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic