UONGOZI wa Mtibwa Sugar umeweka wazi kuwa ulimgharamia kila kitu kinachohusu usafiri na maelewano yalikuwa ni asilimia 99 kwa Hitimana Thiery kusaini ila mambo yaligeuka.
Hitimana ambaye aliwahi kuinoa Namungo FC, Mtibwa Sugar pia alipata zali la kurudi Bongo kwa mara nyingine na ni Mtibwa Sugar iliyo na makazi yake pale Morogoro walisimamia shughuli nzima.
Alipowasili Tanzania akitokea Rwanda alipata muda wa kuzungumza na mabosi wa Mtibwa Sugar na kufikia makubaliano mazuri kabla ya kusaini tu unaambiwa simu moja kutoka kwa mabosi wa Simba ilimzuia kumwaga wino.
Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru akizungumza na Saleh Jembe amesema kuwa hamna namna nyingine zaidi wanatafuta mbadala wake na wamepokea maombi mengi kwelikweli.
"Tulimleta nchini Hitimana na gharama zote za usafiri zilikuwa juu yetu lengo ilikuwa ni kumpa mkataba kwa ajili ya kuifundisha timu yetu hasa ukizingatia kwamba alikuwa anaitambua.
"Kabla ya kumwaga wino katika timu yetu akaondoka na kwenda huko ambako ametangazwa hamna tatizo sisi tunaangalia namna ya kumpata kocha mwingine,".
Mtibwa ilikuwa na Badru Mohamed ambaye aliibuka huko akitokea Gwambina hajapewa mkataba mpya kwa ajili ya kuinoa timu hiyo ambayo inatumia wazawa kwa asilimia 100.
Poleni Mtibwa japo ninyi ni tawi la Simba tu hamna lolote.
ReplyDeleteAlikuwa hana mkataba na Mtibwa hilo ndilo kosa la Mtibwa ingawa Mtibwa na Simba ni watu wenye mahusiano mazuri kama si undugu wa karibu kutokana na hao wahusika wa juu wa Mtibwa ni watu wa Simba vile vile, nnavyoamini hakuja haribika kitu Mtibwa watapata kocha bora zaidi na Simba ni wawakilishi wetu waaminifu kwenye mashindano ya kimataifa wakiimarika zadi wataendelea kutetea zile nafasi nne za ushiriki Africa maana hao wengine wameshaanza kutepeta mapema tu.
ReplyDelete