September 3, 2021


 KAMBI ya Polisi Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu inatarajiwa kuwa Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2021/22.

Taarifa rasmi iliyotolewa na uongozi wa Polisi Tanzania umeweka wazi kuwa maandalizi hayo yatajumuisha na mechi za kirafiki.

Ni jumla ya wachezaji 24 na viongozi 6 wa benchi la ufundi tayari wameondoka mkoani Kilimanjaro kwenda Jijini Mwanza kwa ajili ya kambi ya maandalizi kabla ya kuanza kwa ligi kuu msimu wa 2021/2022

Wachezaji wengine watano watajiunga na timu ikiwa Mwanza ambao kwa sasa wana ruhusa maalum ambao ni Mohmmed Mmanga, Juma Ramadhani, Daruweshi Saliboko na Metacha Mnata.

Ikiwa Mkoani Mwanza timu ya Polisi Tanzania inatarajia kucheza michezo ya kirafiki isiyopungua minne.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic