September 3, 2021


WAWAKILISHI wa Tanzania kwa upande wa Wanawake, Simba Queens leo wameibuka na ushindi wa mabao 10-0 dhidi ya FAD FC.

Katika mchezo wa leo ambao ni wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa upande wa Wanawake, Simba Queens walitakata mapema kwa kuweza kutawala na kutumia nafasi ambazo walitengeneza.

Mpaka muda wa mapumziko ni mabao 7 kwa Simba na kipindi cha pili walifunga mabao matatu na kukamilisha idadi ya mabao 10 kwenye mchezo huo.

Watupiaji wa mabao ya leo ilikuwa ni Mawete Musolo aliyetupia mabao matatu,Opah Clement mabao matatu, Aisha Juma mabao mawili,Asha Djafar mabao mawili.


5 COMMENTS:

  1. Hongera yao lkn FAD ??? ya wapi maliza maelezo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Usishangae kukuta hata muandishi mwenyewe hajui ni ya wapi

      Delete
  2. Hongeren sana dada zangu kwa mauaji kama hayo

    ReplyDelete
  3. Simba ni chama kubwa tunashinda kwa wanaume pia hata kwa wadada zetu wako vyema sana hadi raha

    ReplyDelete
  4. Yanga mnasubiri nn mpaka mbebwe nahuku?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic