CRISTIANO Ronaldo moja ya wachezaji wenye uwezo mkubwa uwanjani na mpambanaji asiyekata tamaa katika timu yake ya taifa ya Ureno amefikisha jumla ya mabao 111 akivunja rekodi kibao na kuwa mfungaji bora wa muda wote kwa timu za taifa.
Nyota huyo rekodi hiyo ambayo ameiweka ni katika mechi 180 ambazo ni dakika 16,200 akiwa na wastani wa kucheka na nyavu kila baada ya dakika 145.
Awali rekodi zinaonyesha kuwa kinara wa mabao kwa timu ya taifa alikuwa ni Ali Daei raia wa Iran mwamba huyu alitupia jumla ya mabao 109.
Mabao ambayo alifunga nyota huyo alikuwa anafunga kwa mitindo mbalimbali mpaka akaweza kufikisha jumla ya namba 11 ambayo sio kazi nyepesi na amesisitiza kwamba bado anataka kuendelea kufunga.Uwezo wake mkubwa ni kwenye mguu wa kulia katika kufunga lakini hata ule wa kushoto nao amekuwa akitumia bila kusahau kichwa katika kumaliza yale mabao yake ya juu.
Rekodi zinaonyesha kwamba kwa mguu wa kulia alipachika jumla ya mabao 58 ambayo ni mengi kuliko yale aliyotumia kufunga kwa kichwa pamoja na ule mguu wa kushoto.
Mguu wa kushoto alitupia jumla ya mabao 25 na alifunga mabao 28 kwa kutumia kichwa alipokuwa ndani ya uwanja na jezi yake ya timu ya taifa.
Pia amekuwa akitupia eneo lolote awe ndani ya 18 ama nje ya 18 anafunga tu ambapo akiwa ndani ya 18 alitupia mabao 90 nje ya 18 mabao 21.
Mreno huyo mwenye miaka 36 ni mkali pia wa kupiga mapigo huru ambapo alifunga jumla ya mabao 10
na alifunga mabao ya penati 14 na alifunga pia jumla ya Hat trick 9.
0 COMMENTS:
Post a Comment