September 10, 2021


 UONGOZI  wa Simba umeweka wazi kuwa kila kitu kwa sasa kuelekea kwenye Simba Day kipo sawa huku Klabu ya TP Mazembe ikithibitisha ushiriki wake na kuwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha lao.

Tamasha la Simba Day linatarajiwa kufanyia Septemba 19, Uwanja wa Mkapa ambapo inatarajiwa kuwa ni siku ya utambulisho wa uzi mpya, wachezaji watakaotumika ndani ya kikosi hicho kwa msimu wa 2021/22.

Tayari rasmi Simba imeitangaza Klabu ya TP Mazembe kutoka Congo kuwa kwenye tamasha hilo ambapo watacheza mchezo wa kirafiki, Uwanja wa Mkapa.

Kaimu Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na wanaamini kwamba watawapa burudani mashabiki wa timu hiyo.

"Hakuna shabiki ambaye hapendi kuona vitu vizuri na Simba ni timu kubwa lazima mambo yetu yawe kwa ajili ya mashabiki na kuonyesha kile ambacho tunacho.

"Kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Simba Day tunaamini kwamba tutafanya vizuri. Mashabiki ni muda sasa wa kununua uzi mpya ambao upo madukani, unapatikana kwenye maduka yote ya Vunja Bei.

"Timu ambayo inacheza na Simba ni kubwa na sababu ya kufanya hivyo ni kuonyesha kwamba nasi tunajipambanua kwa namna ambavyo tupo. Ipo wazi mashabiki ni watu wa muhimu tunawategemea.

"Tutakuwa na wiki ya Simba Day ambayo itaanza Septemba 13 mpaka siku ya tamasha yenyewe na katika muda huu kutakuwa ni muda wa kufanya matendo ya kijamii," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic