September 10, 2021

 


WANAJESHI wa mpakani, Biashara United leo wanakibarua cha kusaka ushindi mbele ya FC Dikhil ya Dijibout utakaochezwa Stade du Ville.


Mchezo huo utachezwa leo Septemba 10, saa 9:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki. 


Kwa mujibu wa Katibu wa Biashara United,  Haji Mtete amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo huo na watapambana kupata matokeo chanya.


"Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya FC Dikhil na tunajua kwamba haitakuwa kazi rahisi tutafanya vizuri,".


Biashara United ya Mara ni mara yao ya kwanza kushiriki mashindano ya kimataifa baada ya kumaliza ligi ikiwa nafasi ya nne.


5 COMMENTS:

  1. Kila la kheri wanajeshi.... Ila mwandishi saa 9 sio jioni

    ReplyDelete
  2. Biashara ni imara na kila na kila ikikipiga itazidi kungara

    ReplyDelete
  3. Mechi je itaoneshwa,? Na kituo gani

    ReplyDelete
  4. Wakati mwingine timu ndogo zijifunze kupitia timu kubwa kama yanga na simba utaendaje kwa mpinzani wako siku moja kabla ya mechi???!!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic