MABINGWA mara tano wa Ligi ya Mabingwa Afrika, TP Mazembe wanatarajiwa kutua rasmi leo Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa kesho, Septemba 19, Uwanja wa Mkapa.
Mbali na kutwaa taji hilo kubwa Afrika mwaka 1967,1968,2009,2010 na 2015 pia timu hiyo ilitwaa mataji mawili ya Kombe la Shirikisho ilikuwa ni 2016 na 2017 itapimana ubavu na Simba.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kaimu Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga amesema kuwa mipango ipo sawa na timu hiyo itawasili hivyo mashabiki wasiwe na mashaka.
“Taratibu zote zipo tayari kuanzia masuala ya tiketi mpaka mapokezi hivyo wale ambao wanamashaka juu ya ujio wa TP Mazembe waache watakuja na mpira utachezwa kama kawaida,” amesema Kamwaga.
Pia Simba walitoa taarifa kuhusu kushughulia usumbufu wa upatikanaji wa tiketi ambao umekuwa ukijitokeza kwa mashabiki wao katika harakati za kukata tiketi hizo.
Leo bado wanaendelea na shughuli za kijamii kwa kufanya matendo ya huruma kwa jamii.
0 COMMENTS:
Post a Comment