September 12, 2021

WAPINZANI wa Azam FC, Horseed FC kutoka Somalia wameweka wazi kuwa walizidiwa mbinu na wapinzani wao Azam FC katika mchezo wa hatua ya awali katika Kombe la Shirikisho uliochezwa Uwanja wa Azam Complex Septemba 11.

 Baada ya dakika 90 kukamilika ubao wa Azam Complex ulisoma Azam FC 3-1 Horseed FC. Kocha Mkuu wa Horseed FC, Mohamed Hussein Ahmed amesema kuwa haikuwa bahati yao kushinda mchezo huo uliokuwa na ushindani. 

 Vivier Bahati, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa kiungo Idd Seleman alikuwa anatengeneza nafasi nyingi ila hazikufika mahali alipokuwa anataka tofauti na wakati anacheza na Prince Dube ambaye Septemba 11 hakuwa kwenye benchi kwa kuwa bado anasumbuliwa na majeruhi.

Mabao ya Azam FC yalifungwa na Ayoub Lyanga dakika ya 32, Idris Mbombo dk ya 73 na Lusajo Mwaikenda dakika ya 76 na lile la Horseed FC likipachikwa na Ibrahim Nor kwa pigo huru dakika ya 22.

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic