September 19, 2021

 


WAWAKILISHI wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa, Yanga leo jitihada zao za kupindua meza kimataifa zimekwama nchini Nigeria kwa kuwa wamefungwa tena.

Yanga ilikuwa na kazi ya kusaka ushindi wa zaidi ya bao 1-0 kwa kuwa katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ilikubali kupoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Leo pia ugenini nchini Nigeria Yanga imepoteza kwa kufungwa bao 1-0 hivyo wametolewa kwa jumla ya mabao 2-0.


Safari yao na malengo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika yameyeyuka mazima hivyo wanarudi Dar es Salaam.

Haji Manara,  Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wamefanyiwa vitendo vya kihuni na wapinzani wao hasa kwenye suala la vipimo vya Corona.


"Tumefanyiwa mambo ya kihuni na tumepewa matokeo ya Corona dakika 45 kabla ya mchezo huu ni uhuni,".

16 COMMENTS:

  1. Kwani mchezaji wao marana hakucheza tena leo wamefungwa

    ReplyDelete
  2. Tamasha letu leo limefana maana tumepigwa kamoja tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tofautisha mechi ya kirafiki na mechi ya kimashindano. Nadhani Utopolo wamepata maumivu makali sana kuishia hatua ya awali ya mashindano ya CAF Champions League

      Delete
    2. Mechi ya kirafiki Ni mechi ya Mazoezi hiyo Ni nzuri Na kosa la golikipa halitakuwepo tena Tarehe 25/9/2021

      Delete
  3. Ile ya Simba ilikuwa ni mechi ya kujipima ili ijuwe wapi ipo sawa na wapi inahitaji marekebisho. Kwa ujumla Simba imeonesha kiwango kikubwa kubwa sana cha uwezo na ufundi dhidi ya timu kubwa sana Afrika iliyochukuwa makombe ya klabu bingwa Africa mara nne na kuziwezeshana timu nyengine kadhaa kushiriki mashindano kama hayo. Hongera Simba

    ReplyDelete
  4. Mulisemaje tulipofungwa na zanaco,laana itawatafuna tu,tunawasubiria klabu bingwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Zanoco klub za afrika sijui ni ya ngap simba amecheza na mkubwa mwenzake nyie utopolo tumechoka kuwabeba kila tukiwabeba mnatuangusha

      Delete
    2. Niwape ushauri YANGA kwa mwakani msishiriki KOMBE LA KIMATAIFA LOLOTE BALI JENGENI TIMU KWANZA ,SASA MUMESAJILI MSEMAJI BADO WACHEZAJI

      Delete
    3. Laana ya Yanga kufungwa ilianzia KIGOMA KWENYE MACHOZI NA SIMBA KUIBUKA BINGWA.
      Tarehe 25/9/2021
      Jitahidi msifungwe Maana mkifungwa tu mtaingia kwenye ligi Na Laana ,japo kwa mahesabu ya kawaida YANGA inastahili kufungwa Tarehe 25/9/2021 kuanzia GOLI MBILI NA KUENDELEA

      Delete
  5. Wewe huoni aibu kuifananisha TP Mazembe na Zanaco iliyo kufungeni, timu ambayo haina historia yoyote ya kufanya makubwa kama ilivo Mazenbe na Simba.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mimi naona tuwapongeze Yanga wametimiza malengo ya kusafiri kwenda nje ya Nchi Mara mbili yaani Morocco Na Nigeria. Big up YANGA

      Delete
  6. Ama uwezo wa aliouonesha Mnyama jana mbele ya timu namba mbili Mazembe baada ya Al Ahli umeturidhisha sana sana na roho zetu safi kabisa na iliyobaki pinduwa meza yamekwisha na tunangoja porojo jipya na hiyo tarehe 25

    ReplyDelete
  7. Nimesikia MSEMAJI wa YANGA akisema wamefanyiwa uhuni vyumba vya kubadilishia nguo vilikuwa Na Giza !!!!
    Sasa najiuliza nguo walienda nazo au walienda kuzitafutia vyumbani??
    Je ukibadilushia nguo kwenye Chumba cha Giza kunakufanya ufungwe b???
    Sababu hizo zinatosha ???
    Tarehe 25/9/2021 sababu zitakuwa zipi ???

    ReplyDelete
  8. Ila walisajili wafungaji na watakaoleta makombe!! Sasa hivi visingizio vya kutoingiza timu uwanjani vinatoka wapi? Walijisahau kumshangilia Manara badala ya kujenga timu.

    Timu za kwenye Media hazipo siku hizi, mpira ni dakika 90. Oneni Biashara hawajaongea kitu ila wamefanya yale yanayowahusu. Ooooh jezi, mara wanalia na Manara, mara wameuza wachezaji mara Luis anaibukia Yanga kikuwapi?

    Mara Makambo amekuja kuondoa ukame wa mabao Yanga nk

    ReplyDelete
  9. Timu maendeleo yako hayaji kwa kumkomoa jirani yanga walifikiri kumchukua CEO na msemaji wa simba inatosha kuwa na timu bora badala ya kuangalia simba wanachofanya kupata matokeo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic