WANAJESHI wa mpakani, Biashara United, leo Oktoba 13 wameendelea kuwavutia kasi wapinzani wao katika mchezo wa Kombe la Shirikisho unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
Itakuwa ni Oktoba 15, Ijumaa dhidi ya Al Ahly Tripoli ya Libya na ule wa marudio unatarajiwa kuchezwa nchini Libya.
Wachezaji wote wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Miongoni mwa mastaa ambao walikuwepo mazoezini leo ni pamoja na Redondo, kipa namba moja James Ssetuba, Duchu.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Biashara United, Seleman Mataso amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya kupata matokeo chanya.
0 COMMENTS:
Post a Comment