HONGERENI Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake, Twiga Stars kwa kupeperusha bendera nchini Afrika Kusini na kuweza kutwaa taji la COSAFA 2021.
Wanawake mmeweza kuipeperusha bendera ya Tanzania na kuonyesha kwamba kila kitu kinawezekana kwenye ulimwengu wa mpira na hilo ni jambo kubwa na linastahili pongezi.
Benchi la ufundi ambalo lipo chini ya Kocha Mkuu, Bakari Shime ni kuona kwamba kila mmoja anatimiza majukumu yake na ipo wazi kwamba ushindani ulikuwa mgumu na haikuwa rahisi kufika hapo.
Kwa namna ambavyo Twiga Stars mmepambana mnatoa picha kwamba uwekezaji kwenye Ligi ya Wanawake nao unahitaji nguvu zaidi ili kuweza kupata matunda zaidi ya hapa.
Imekuwa ni kasumba kwa timu zetu zinafanya vizuri zikitoka nje ila zikiwa nyumbani kwa zile za chini ya miaka 20 kwa miaka ya hivi karibuni zilikuwa zinaboronga hivyo kwa mwendo ambao unaendelea kwa sasa inaonyesha kwamba kila kitu kinazidi kuwa imara.
Pongezi kwenu kwa kufanya vizuri kwani haikuwa kazi rehisi ninarudia tena lakini ni majukumu yenu na mmetimiza bila kuogopa hongereni na mnastahili pongezi.
Kilicho nyuma ya ushindi ndani ya uwanja ni lazima kila mmoja afanye kazi kwa juhudi na inawezekana kwa kuwa kila mmoja anahitaji kushinda.
Pia kwa ile timu ya taifa ya Tanzania chini ya 20 nayo iliweza kufanya vizuri kwenye mchezo wao wa kufuzu Kombe la Dunia ambao ulichezwa Uwanja wa Azam Complex.
Ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ertrea nao si haba kwa kuwa inaonyesha kwamba nanyi mnatambua kwamba taifa linapenda kuona mkifanya vizuri katika hilo hongereni.
Kazi inabidi iendelee kwa kuwa bado mashindani yapo na mechi zinazokuja ni ngumu kuliko hizi ambazo zinapita maana yake ni kwamba nguvu inahitajika zaidi ili kuweza kupata matokeo mazuri zaidi.
Ukiachana na hilo pia inabidi tukumbushane kuhusu mwendo wa ligi ambayo inatarajia kurejea hivi karibuni baada ya kusimama kwa muda.
Hapa nikianza kuangilia ile Championship namna inavyokwenda na ushindani ulivyo mkubwa na huku pia ni muhimu kuwekeza nguvu kubwa.
Katika Champinoship tunasema huku ni kiwanda cha kutengeneza vijana wa kesho na ili waweze kufanya vizuri ni lazima ushindani wao uwe mkubwa na maisha yao pia yawe yenye ushindani.
Ipo wazi kwamba kupanda ni rahisi licha ya kwamba kuna ushindani lakini ukishuka kurudi ni wimbo mwingine ambao ni mgumu kuimbwa na kupendwa pia na wenye timu Bongo.
Kwa timu ambazo zimepanda bado zinapaswa kukumbuka pongezi ambazo wanapewa kwa wakati huu ni lazima wazilipe kwa kufanya kazi kwa vitendo uwanjani.
Kupitia kwa wale ambao walipanda na kushuka basi kuwape nguvu ya kupambana wale ambao wamepanda na wasisahau kwamba kuna suala la kushuka pia.
Tunataka kuona timu ikipanda kwenye ligi iwe na uwezo na vigezo vya kuhimili mikikimikiki ya huku kwani hakuna kuzubaa ni mwendo wa kukimbizana mwanzo mwisho.
Kila timu ifanye kazi kwa kushirikiana katika kusaka mafanikio na hiyo itaongeza nguvu kwa kila mchezaji kuweza kupata ushindi na kufanya mabo ambayo ni ya tofauti.
Maandalizi mazuri ni siri ya ushindi na kushirikiana katika kila jambo ni muhimu kwa ajili ya wakati huu ndani na nje ya uwanja.
Hakuna ambaye anapenda kuona timu yake inashindwa kupata matokeo chanya ama hakuna ambaye anapenda kuona kwamba timu yake inashuka.
Ushindi haupatikani kwa wepesi lazima utafutwe kwa ushindani na wale ambao wanahitaji ushindi hivyo lazima juhudi iwepo.
Hakuna kinachoshindikana kwenye ulimwengu wa mpira jambo la msingi ni maandalizi mazuri.
0 COMMENTS:
Post a Comment