NYOTA wawili wa kikosi cha Simba ambao ni mshambuliaji Chris Mugalu na kiungo Osmane Sakho kuna hatihati wakaukosa mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Oktoba 17 nchini Botswana na mpaka sasa nyota hao bado wapo kwenye uangalizi maalumu kabla ya kujiunga na wachezaji wenzao katika mazoezi.
Mugalu jana hakuwa kwenye mazoezi ya timu baada ya kupumzishwa huku Sakho akiendelea kuwa kwenye program maalumu ili aweze kurejea kwenye ubora.
Ikumbukwe kwamba Mugalu aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji sawa na mshikaji wake Sakho.
Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa Mugalu ni moja ya washambuliaji wazuri lakini kwa sasa bado anapambania afya yake hivyo imani yao ni kumuona akirudi kwenye ubora.
“Bado Mugalu hajawa fiti kwa sasa ila taratibu anarejea kwenye ubora, kwa upande wa Sakho naye pia anaendelea vizuri hivyo bado tunaamini kwamba watarejea katika majukumu yao hivi karibuni,” amesema.
Wapuuzi wamewavurugia wenzao kibarua chao.
ReplyDeletesakho kesho ajiunga mazoezin
ReplyDeletePoleni sana.Iam Esperius
ReplyDeletemungu atawasimamia watalejea tu kwenye majukumu yao
ReplyDelete