October 13, 2021


 IMEBAINISHWA kuwa, video za mechi za wapinzani wa Simba katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Jwaneng Galaxy, zitaamua aina ya kikosi ambacho kitaanza kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 17, mwaka huu.


Habari kutoka Benchi la Ufundi la Simba, zimeeleza kuwa, baada ya Kocha Mkuu, Didier Gomes kupata video za wapinzani wao, walikaa kikao kujadili namna ya kuwakabili.

Kupata video hizo ni sawa na kupata mbinu za wapinzani hao ambao watakutana na Simba kwenye mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkali.

“Haikuwa kazi rahisi kupata video zao za hivi karibuni kwani inaonekana hawajacheza muda mrefu, lakini kwa zile ambazo zimepatikana zilitazamwa kwa umakini na baada ya kutazamwa kikao ilibidi kifanyike kuwajadili wapinzani wetu.


“Kikao hicho kiliamua aina ya wachezaji ambao wataanza kwenye mchezo ujao ila kwa sasa ambacho kinatazamwa ni kurejea kwa wachezaji kutoka kwenye majukumu yao ya timu za taifa pamoja na wale ambao ni majeruhi,” ilieleza taarifa hiyo.


Kuhusu wapinzani hao, Gomes aliliambia Spoti Xtra kuwa: “Kutazama video pekee haitoshi kusema kwamba mchezo tumemaliza, bado kazi ipo lakini kwa kujua namna ambavyo wanafanya itatupa mwanga wa nini tunakwenda kufanya.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic